Na Pamella Mollel - Jamiiblog
Taasisi na Makampuni mbalimbali zimeshauriwa kuzijali Jamii zinazowazunguka kwa kutoa
michango yao ili kuziwezesha kutambulika vyema ndani ya jamii lakini
pia Jamii kuthamini mchango wa Kampuni na huduma inayozitoa.
Wakizungumza
kwa Nyakati tofauti Wakazi wa Jiji la Arusha walisema kuwa Makampuni
mengi ndani ya Jamii yameshindwa kutambulika kutokana na kutothamini
jamii zinazowazunguka kwa kutokukutana nao wala kuchangia huduma muhimu
za Jamii kama huduma za Afya,Elimu na Maji.
Jumanne Manjano Mkazi wa Majengo alisema kuwa ikiwa kama Taasisi na Makampuni zitawafuata wananchi walipo
basi ni wazi kuwa Jamii zilizopo katika maeneo yao zitaweza kunufaika
na kupata faida kutokana na kuona thamani ya Kampuni husika katika Jamii
yao.
Manjano
ambaye pia ni mmoja wa Washindi wa Kampeni ya Kapu la Pasaka
inayoendeshwa na kituo cha Redio 5, kilichopo Jijini hapa wameshukuru
kampuni hiyo kwa kuijali Jamii inayowazunguka kwa kurudisha faida kwa
Jamii kwa kuwafuata walipo.
“Ninafurahia
sana zawadi hii nikiwa kama mmoja wa wasikilizaji wa Redio 5 hata
hivyo nina uhakika wa kusherehekea vyema Sikukuu ya Pasaka mimi na
familia yangu kwa kuwa kapu hili limejaa mahitaji yote muhimu kwa ajili
ya sikukuu ukizingatia vitu vinapanda bei sana msimu huu”alisema Manjano
Magreth
Suleiman Mkazi wa Mbauda Arusha alisema kuwa ni vyema Taasisi
nyingine ambazo zinatoa huduma kwa jamii kuziwezesha Jamii
zinazowazunguka ili kujenga ushirikiano lakini pia jamii kuthamini
mchango wa Taasisi hizo na huduma wazatoa.
Hata
hivyo alisema kuwa kutokana na ugumu wa maisha sikukuu za sasa zimekosa
mwamko kwa kuwa wananchi wanashindwa kumudu gharama za mahitaji muhimu
kama vyakula kutokana na kupanda katika msimu wa sikukuu.
Kwa
upande wake msimamizi wa vipindi katika kituo hicho Mathew Philip
alisema kuwa kampeni hiyo ni hamasa kwa wasikilizaji na wakazi wa Jiji
la Arusha na viunga vyake,ambapo kampuni hiyo imeamua kurudisha faida
kwa Jamii, ambapo wanapata fursa ya kujishindia mahitaji muhimu.
Alifafanua
kuwa ndani ya kapu hilo kuna vyakula kama mchele,Mafuta ya Kupikia,Unga
wa Ngano,Chumvi,Masala,Majani ya chai,Maziwa,Sukari lengo likiwa ni
kumrahishia mshindi kupata mahitaji muhimu ili kusherehekea vyema
sikukuu ya Pasaka yeye na familia yake.
Mathew
alisema kuwa kampeni ya kapu la Pasaka ni muendelezo wa kampeni ya Nipe
Tano inayoendeshwa na kituo hicho lengo likiwa ni kurudisha faida kwa
jamii lakini pia kudumisha Upendo,Amani na Mshikamano.
No comments:
Post a Comment