Mafuru hakupanda ulingoni katika mashindano ya Jumuiya ya Madola ambayo yalimalizila Agosti 3, huko Glasgow, Scotland kwasababu walizodai kwamba alishikwa na tumbo la kuharisha.
Mafuru alisema kwa njia ya simu jana, kuwa alikuwa mzima na hajawahi kuumwa tangu walipofika katika mashindano hayo, na kwamba walichelewa kufika eneo ukumbini viongozi ambao aliongozana nao ndio waliotoa sababu za kuugua.
“Mimi sikuugua nilikuwa mzima, lakini tulichelewa kufika ukumbini nilikuwa nishajiandaa baada ya kufika tukakuta wanamtangaza bingwa Yule ambaye nilitakiwa kucheza naye lakini nawashangaa waliosema kwamba nilikuwa naumwa wakati tulikuwa na daktari ambaye naye hakujua kuumwa kwangu,” alisema Mafuru.
Aidha, Mafuru alisema kuna wanaosema kwamba alikosa kocha wa kumpandisha ulingoni, kwamba kwasababu walichelewa kufika hata kocha ambaye alitakiwa kumpandisha naye akawa kashaondoka.
Mafuru aliwataka Watanzania kutomfikiria kwamba alikuwa anaogopa ushindani katika mashindano hayo, si hivyo kwani alijiandaa na alikuwa na uhakika wa kufanya vizuri katika mashindano hayo.
Chanzo: Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment