ZIARA KIMATAIFA : DKT. ALI MOHAMED SHEIN YUKO ZIARANI NCHINI INDIA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Sunday, 2 February 2014

ZIARA KIMATAIFA : DKT. ALI MOHAMED SHEIN YUKO ZIARANI NCHINI INDIA


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Ujumbe wake wakiongozana na Balozi wa Tanzania Nchini India John W.H.Kijazi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa  Indra Gandhi,Rais atakua nchini India kwa ziara rasmi ya siku tisa.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na akizungumza na Balozi wa India nchini Tanzania  Debnath Shaw katika ukumbi wa VIP wa  uwanja wa ndege wa Kimataifa wa  Indra Gandhi Nchini India Rais akiwa huko atatembelea sehemu mbali mbali ikiwa ni katika kukuza Uhusiano na mashirikiano ya kiuchumi na Kijamii.
 Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi Juma Maalim,ni miongozi mwa ujumbe wa Rais wa Zanzibar katika safari rasmi nchini india,hapa wakiwa katika ukumbi wa VIP wa  uwanja wa ndege wa Kimataifa wa  Indra Gandhi Nchini India ambapo  utatembelea sehemu mbali mbali ikiwa ni katika kukuza Uhusiano na mashirikiano ya kiuchumi na Kijamii.
 Baadhi ya raia wa nchini India, wakisimama barabarani kuushangaa msafara wa Rais wa Zanzibar, akiwa ziarani nchini India. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na ujumbe wa walikaribishwa kwa ngoma za asili mara baada ya kufika katika hoteli ya Oberoi Taj Vilas,katika jimbo la Rajastani Nchini India Rais akiwa huko atatembelea sehemu mbali mbali ikiwa ni katika kukuza Uhusiano na mashirikiano ya kiuchumi na Kijamii.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  na ujumbe aliofuatana nao wakipata maelezo kutoka kwa Kiongozi Panraj Dharendra,katika Sehemu ya Historia inayoitwa Amber,wakati alipotembelea sehemum hiyo maarufu katikan jimbo la Rajastan Nchini India,akiwa huko Rais atatembelea Taasisi mbali mbali  ikiwa ni katika kukuza Uhusiano na mashirikiano ya kiuchumi na Kijamii.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  na ujumbe aliofuatana nao wakipata maelezo kutoka kwa Kiongozi Panraj Dharendra,katika Sehemu ya Historia inayoitwa Amber,wakati alipotembelea sehemu  hiyo maarufu katikan jimbo la Rajastan Nchini India,akiwa huko Rais atatembelea Taasisi mbali mbali  ikiwa ni katika kukuza Uhusiano na mashirikiano ya kiuchumi na Kijamii.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akitia saini kitabu cha wageni wanaotembela  Sehemu ya Historia inayoitwa Amber, maarufu katika jimbo la Rajastan Nchini India,RAIS akiwa huko  atatembelea Taasisi mbali mbali  ikiwa ni katika kukuza Uhusiano na mashirikiano ya kiuchumi na Kijamii. Picha na Ikuulu

No comments:

Post a Comment