Matukio :Taswira ya Mazishi ya Brigedia Jenerali (Mstaafu) Hashim Mbita katika makaburi ya Kisutu, jijini Dar - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 30 April 2015

Matukio :Taswira ya Mazishi ya Brigedia Jenerali (Mstaafu) Hashim Mbita katika makaburi ya Kisutu, jijini Dar

Viongozi mbali mbali wa Dini ya Kiislam wakishiriki pamoja na waumini wao kwenye Ibada ya kuuswalia mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita kwenye Msikiti wa Mtoro, Kariakoo na baadae kwenda kuuhifadhi kwenye nyumba yake ya milele, Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam.Picha zote na Hamis Makuka.
 Maelfu ya waunini wa kiislam wakishiriki kuubeba mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita wakati wakiutoa kwenye Msikiti wa Mtoro, Kariakoo na tayari kwa kwenda kuuhifadhi kwenye nyumba yake ya milele, Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wakiongoza shughuli ya kuusafirisha mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita kuelekea kwenye nyumba yake ya milele, Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam
Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali (Mstaafu) Hashim Mbita, ambaye amezikwa kwa heshima zote za kijeshi na kwa taratibu ya dini ya Kiislam kwenye Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam
 Mwili umewasili makaburuni tayari kwa Mazishi.
 Shuguli na taratibu zote za Mazishi zikiendelea.
 Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo Kaburini.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange akiweka udongo Kaburini.
Viongozi mbali mbali walioshiriki kwenye Mazishi ya Marehemu Brigedia Jenerali (Mstaafu) Hashim Mbita.

No comments:

Post a Comment