Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi msaada wa
Vipaza sauti Amiri wa Jumuiya ya Sherehe za Siku Kuu ya Iddi Matemwe
Ustaadhi Kundi Choum Haji kutekeleza ahadi aliyoip[a Jumuiya hiyo wakati
wa sherehe za siku kuu ya Iddi el Hajj iliyopita.
Mke
wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi
akimkabidhi mchango wa Shilingi 400,000/- kwa kila kikundi miongoni
mwa vikundi 14 vya Ushirika wa Akina Mama vilivyomo ndani ya Wilaya ya
Kaskazini “ A “.
Balozi
Seif akikabidhi Seti moja ya Jezi na Mipira kwa kila Timu ya Soka
miongoni mwa timu nne zilizomo ndani ya Jimbo la Matemwe.
Balozi
Seif akiangalia hodhi linalojengwa kwa ajili ya kuhifadhia maji kwenye
Msikiti Mkuu wa Kijiji cha Mvuleni Kidoti Jimbo la Nungwi Mkoa wa
Kaskazini Unguja.
Balozi
Seif akiuagiza Uongozi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Kijiji cha Mvuleni
kufanya Tathmini ya uenzi wa Vyoo ili uwahi kufunguliwa katika muda
muwafaka uliopangwa.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewakumbusha Wananchi
hasa akina Mama Nchini kuwaunga mkono Viongozi wenye muelekeo wa
kuwasimamia vyema katika harakati zao za Maendeleo, kiuchumi na ustawi
wa Jamii.
Alisema
takwimu ya idadi ya watu Nchini inaoonyesha wazi kwamba Wanawake ndio
wenye uwezo wa kutumia kura zao katika kuchaguwa Viongozi watakaowafaa
kwenye maeneo yao kutokana na wingi wao.
Balozi
Seif Ali Iddi alitoa kumbusho hilo wakati akikabidhi Vipaza Sauti kwa
ajili ya Jumuiya ya Kuhifadhi Quran pamoja na Sherehe za Siku Kuu ya
Kiislamu ya Kijiji cha Matemwe Wilaya ya Kaskazini “A” Mkoa wa
Kaskazini Unguja akitekeleza ahadi aliyoitowa wakati wa Siku Kuu ya
Mfunguo Tatu uliopita akiwa mgeni rasmi.
Balozi
Seif alisema huu ni mwaka muhimu kwa Taifa la Tanzania ambapo Wananchi
wanapaswa kuwa makini katika kufanya uamuzi muafaka wa kura ya maoni
pamoja na uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba.
Alisema
uwamuzi wa Wananchi hao endapo hautazingatia hatma yao ijayo ya miaka
mitano kwa kuchaguwa viongozi makini na imara wasijetafuta visingizio
vya lawama kwa viongozi watakaowaweka madarakani.
Mapema
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi
akitekeleza ahadi yake ya kuviwezesha Baadhi ya Vikundi vya Ushirika
vya akina Mama wa Wilaya ya Kaskazini “A “ alisisitiza umoja na
mshikamano miongoni mwa Wananchi wa Wilaya hiyo.
Mama
Asha alisema mshikamano huo ndio njia pekee itakayowawezesha wananchi
hao kuendelea na shughuli zao za kujitafutia riziki katika hali ya amani
na utulivu.
Alitanabahisha
kwamba yapo Mataifa kadhaa duniani yakiwemo yale ya Bara la Afrika
ambayo baadhi ya wananchi wake walijaribu kuichezea amani na hivi sasa
tayari wameshatumbukia katika dimbwi la vurugu zilizozaa maafa
yaliyoacha makovu yatayoendelea kukumbukwa milele na Mataifa hayo.
No comments:
Post a Comment