Afya Zetu : Madaktari wa Moyo kutoka India watoa Huduma ya Matibabu , Jijini Arusha - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 21 April 2015

Afya Zetu : Madaktari wa Moyo kutoka India watoa Huduma ya Matibabu , Jijini Arusha


SAM_2087Mratibu wa Kambi ya matibabu Arusha katika kituo cha kutoa huduma kwawanawake (MMC)kilichopo mkabala na Hoteli ya Impala, ambapo ushauri huo unatolewa, Austin Makani akizungumza na waandishi wa habari  juu ya ujio wa madaktari bingwa kutoka India kwaajili ya kuwaona wagonjwa wenye matatizo ya Moyo,Tumbo,Upasuaji wa saratani,Mishipa ya fahamu na uti wa mgongo,Shida za Figo,Mifupa,upasuaji wa jumla na upasuaji wa kupunguza uzito,zoezi hilo litafanyika kwanzia tarehe20-22
SAM_2071
Madaktari bingwa kutoka India
SAM_2085
Daktari bingwa kutoka India katika hospitali ya Apollo Abhijit Singh akizungumza jambo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha katika kituo cha MMC Health
SAM_2088
Wagonjwa wakiwa wanapatiwa vipimo mbalimbali
SAM_2082
Atul Behll ambaye pia ni daktari bingwa kutoka India akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari
SAM_2097
Mgonjwa aliyekuja kupata huduma akiwa anasaidiwa na wahudumu wa kituo hicho
SAM_2084
Wagonjwa wakiwa wanasubiria kupata huduma
SAM_2091
Mwandishi na Mmiliki wa Blog ya Jamii Pamela Mollel akipata U kodak na Madakatari hao
SAM_2077
Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa kazini
 
Na Woinde Shizza , Arusha
MADAKTARI bingwa kutoka hospitali ya  SPS Apollo iliyopo  Ludhiana nchini India wamewasili nchini na kuanza kutoa huduma ya ushauri bure kwa magonjwa makubwa ambayo yamekuwa yakiwasumbua watu wengi na kuwalazimu  kwenda kutibiwa nchini India.

Akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha kutoa huduma kwa wanawake (MMC) ambapo ushauri huo unatolewa, Mratibu wa Kambi hiyo ya matibabu Arusha, Austin Makani alisema kuwa , madaktari bingwa hao wanatoa ushauri kwa wagonjwa wenye matatizo ya Figo , Moyo, tumbo, saratani, mishipa ya fahamu, uti wa mgongo, upasuaji wa kawaida na wa
kupunguza uzito.

Austin alisema kuwa,  ujio wa madaktari hao watano kutoka  nchini India umeratibiwa na kituo  cha kutoa huduma kwa wanawake (MMC) kwa kushirikiana na hospitali ya SPS Apollo iliyopo Ludhiana nchini India na wamefikia hatua hiyo baada ya kugundua kuwa wagonjwa wengi wanaoenda kutibiwa nchini India wanasumbuliwa na magonjwa hayo.

Alisema kuwa, uwepo wa madaktari hao bingwa kwa siku tatu utasaidia sana wananchi wa jiji la Arusha kufika na kupewa ushauri bure juu ya magonjwa yanayowasumbua na hivyo kuokoa gharama ya kusafiri hadi nchini India kufuata huduma hizo.

‘hapa sisi wanachofanya madaktari hawa bingwa ni kusikiliza wagonjwa na baada ya kupata maelezo wanapata ushauri bure wa kwenda kupima kulingana na ugonjwa alionao na baada ya kurudisha majibu ndipo tunamwandikia dawa ya kutumia na kama ugonjwa wake unahitaji kutibiwa India tunampunguzia  gharama  kidogo ya kwenda kutibiwa India ‘alisema
Austin.

Alisema kuwa, uwepo wa kambi hiyo ya matibabu jijini Arusha unatoa fursa pia kwa wagonjwa waliokuwa wakatibiwe nchini India kutokana na magonjwa yanayowasumbua na kuweza kupata ushauri wa haraka na wakti mwingine kuepuka gharama za kusafiri.

Wakizungumza  katika kituo hicho, Madaktari hao bingwa ,Abhijit Singh na Atul Behll kutoka hospitali ya SPS Apollo India  walisema kuwa ,changamoto kubwa iliyopo katika nchi za kiafrika ni watu wengi kutokuwa na utamaduni wa kwenda kupima afya zao ,hivyo aliwataka
wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani kufika kwa wiki ili kupata ushauri juu ya afya zao.

Walisema kuwa,nchini India  kuna watanzania wengi wanaopata matibabu kutokana na magonjwa yaliyotajwa ,hivyo wakaona kuna umuhimu mkubwa kwa wao kuwafikia na kuweza kutoa ushauri bure na hatimaye kupunguza gharama za kwenda nchini India. Picha na Woinde Shizza Blog

No comments:

Post a Comment