makundi mbalimbali ya kijamii ya mikoa ya Kaskazini, inayojumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Manyara wakiwa wanaandamana kwa pamoja kuelekea kwa mbunge wa jimbo la monduli hii leo |
Katibu wa
Chama cha Wasioona Mkoa wa Kilimanjaro (TLB), Protas Soka
Akisoma risala kwa niaba ya makundi hayo
mbele ya mbunge wa jimbo la monduli
Viongozi mbalimbali wa
makundi ya kijamii wakiwa wanamkabidhi waziri mstaafu ambaye pia ni
mbunge wa jimbo la Monduli Edward Lowasa bahasha yenye fedha taslimu
shilingi milioni mbili laki tano sitini na saba elfu na mia sita
zilizochagwa na wananchi kwa ajili ya kwenda kuchukuwa fomu ya
kugombea nafasi ya Urais
mbunge wa jimbo la monduli akiangalia picha
ambayo ametengenezewa na vijana kutoka makundi wakati
walipomtembelea nyumbani kwake monduli kwa ajili ya kumkabidhi fedha
kidogo kwa ajili ya kuchukuwa fomu ya kugombea urais
makundi
mbalimbali ya kijamii ya mikoa ya Kaskazini, inayojumuisha mikoa ya
Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Manyara wakiwa wanaandamana kwa pamoja
kuelekea kwa mbunge wa jimbo la monduli hii
leo
Mratibu wa Marafiki wa Lowasa Kanda ya Kaskazini,
Noel
Nnko,akiwa anamuonyesha picha ambayo ni ya kumbukumbu ya tukio la leo
la kuja kumuunga mkono mbunge wa jimbo la monduli pamoja na kumuomba
atangaze nia ya kugombea nafasi ya
urais
maandamano ya pikipiki yakiwa yanaelekea nyumbani
kwa mbunge wa jimbo la monduli hii
leo
Na Woinde Shizza,Monduli
Wananachi zaidi
ya 700 kutoka makundi mbalimbali
ya kijamii ya mikoa ya Kaskazini, inayojumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Tanga,
Arusha na Manyara, wamejitokeza nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Monduli (CCM), Edward Lowassa, wakimshawishi atangaze nia ya kugombea
urais kupitia
chama hicho.
Wananchi
hao kutoka katika Makundi mbalimbali katika
ya mikoa hiyo yamewasili leo
nyumbani kwake,Kijiji cha Ngarashi, Wilaya ya Monduli baada ya kufanya
maandamano makubwa yaliyoanzia njia panda ya Monduli, wakiimba nyimbo za
matumaini kwamba 'wewe ni tumaini la walio wengi Tanzania, maamuzi na matumaini
mapya, watanzania wako nyuma yako'.
Aidha
akisoma risala kwa niaba ya makundi
hayo baada ya kuwasili nyumbani hapo ,
Katibu wa Chama cha Wasioona Mkoa wa Kilimanjaro (TLB), Protas Soka
alisema kwa nia thabiti isiyo na kigugumizi asilani, wanaharakati hao pamoja na
watanzania wengine wanamhitaji (Lowassa) kwa unyenyekevu na hivyo,
wanamwomba atangaze nia ya kuingia kwenye kinyang'anyiro cha Urais
mwaka 2015.
"Leo
watanzania tumepaza sauti zetu kwa pamoja kuanzia ngazi ya
Kaya,Kitongoji,Kijiji,Kata, Tarafa,Wilaya, Kanda mpaka Taifa
wakisema Viva
Lowasa, Tobiko Lowasa. Kwa moyo mmoja bila kushawishiwa na mtu wala kikundi
chochote; wanaharakati hawa wamekuona wewe, mheshimiwa Edward Lowasa ndio
kiongozi sahihi kwa mustakabali na manufaa ya taifa letu,"alisema
Soka
Makundi
hayo ambayo ni walemavu, waendesha bodaboda, walimu, wataalam wa afya, vijana
na wanasiasa, walimchangia Lowassa kiasi cha shilingi milioni 2,567,600 kwa
ajili ya kununua au kulipia fomu ya kugombea nafasi ya Urais pindi
atakapotangaza nia.
"Kwa
lugha nyingine sasa tunakuomba Mheshimiwa Lowasa sasa tunakuomba utangaze nia
ya kuingia kwenye kinyang'anyiro cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,"alisema Soka.
Makundi
hayo yaliyoongozwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) mkoa wa Kilimanjaro, Paul Matemu, Mratibu wa Marafiki wa Lowassa Kanda ya
Kaskazini, Noel Nnko,Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa na Mwenyekiti wa Jumuiya
ya Umoja wa Vijana (UVCCM), mkoa wa Arusha, Robnson Meitinyiku, Mjumbe wa
Mkutano Mkuu wa Taifa, Fred Mushi, Askofu wa Kanisa la Calvary Assemblies of
God, Christopher Madilu ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa na Abdalah
Sadick kutoka mkoa wa Manyara.
Akizungumza
mara baada ya kupokea makundi hayo mbunge huyo wa jimbo la monduli alisema kuwa
amekubaliana nao na anatarajia kutangaza rasmi nia mwezi Aprili pindi tu chama
chake kitakaporuhusu
"Nitatangaza nia mwezi Aprili mwaka huu, pale
uwanja wa Shekhe Amri Abeid mjini Arusha baada ya chama changu kupuliza
kipenga. Ninachowaomba watanzania kwa sasa, mniombee katika safari yangu ya
matumaini,"alisema Lowassa.
habari kwa hisani ya libeneke
la kaskazini blog
No comments:
Post a Comment