Matukio : Deo Filikunjombe Ataka Viongozi wa Dini Kuwaombea Wabunge Watimize Ahadi zao - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Monday 16 March 2015

Matukio : Deo Filikunjombe Ataka Viongozi wa Dini Kuwaombea Wabunge Watimize Ahadi zao

Mbunge  wa Ludewa,Deo Filikunjombe  akisisitiza  jambo  wakati  akitoa  salamu  zake kwenye  mazishi ya SR. Instrude maria
Katibu mwenezi wa CCM mkoa  wa  Njombe Bw Honolatus Mgaya kushoto  na  mbunge wa Ludewa  Deo Filikunjombe  kulia  wakishirikiana na wananchi  wa  Njombe  kubeba jeneza na SR. Maria. 
 Mbunge  Filikunjombe katika usikivu mkubwa
 Na Matukiodaima BLoG

Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe amewaomba viongozi wa dini nchini kuendelea kuwaombea viongozi wa serikali wakiwemo wabunge ili kuwatumikia wananchi kwa kutanguliza hofu ya Mungu  ya  kwatumikia  wananchi waliowachagua

Kauli hiyo aliitoa Jana wakati wa mazishi ya aliyekuwa mtawa wa kanisa la Romanikatoliki Parokia ya Imiliwaa Marehemu SR. Insetrud Maria

Alisema kuwa viongozi wa dini wamekuwa wakifanya kazi ya kuliombea Taifa na watu wake ila wanasiasa na viongozi wa serikali wamekuwa wakiwatumikia wananchi kimwili hivyo kuna haja ya viongozi wa dini kuendelea kufanya kazi ya kuwaombea viongozi .


" maandiko matakatifu yanasema kuwa enendeni duniani mkawafanyi watu wote kuwa wanafunzi wangu...chama cha walimu hapa wamesema kuwa SR.Maria alikuwa mwalimu mzuri hivyo ni wazi alizifanya kazi zote ya kiroho na Kimwili "

Hivyo alisema kwa kutambua mchango wake alioutoa hapa duniani Enzi za uhai wake kwa upande wake ameguswa kujenga darasa katika shule ya sekondari parokioni hapo Kama njia ya kumuenzi zaidi.

Filikunjombe alisema kuwa iwapo kitajengwa kitu chochote cha kumbukumbu liwe darasa la shule ya msingi ama sekondari ni kumbukumbu tosha .

Alisema mchango wa SR. Maria katika maendeleo ya mkoa wa Njombe ni mkubwa na kuwa haitapendeza mchango wake huo kuachwa bila kuenziwa.

" SR .Instrud Maria mbali ya kazi yake ya utawa pia alikuwa ni mwalimu na mchango wake katika shughuli zake ni mkubwa hivyo nawaombeni tumienzi kwa kujenga darasa Moja ambalo litaandikwa jina lake Kama kumbukumbu ya sasa na baadae"
Kuwa kwa upande wake atahakikisha darasa hilo linajengwa kwa kupitia uwezo wake na wahisani mbali mbali .

SR.Maria alifariki juzi kwa ugonjwa wa shinikizo la Damu na mazishi yake kuongozwa na askofu wa jimbo la Njombe Alfred Maluma .

walimu  Njombe  wakiimba  wimbo wa  wafanyakazi kabla ya  kuweka  shada

No comments:

Post a Comment