Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama
Mhe Benson Mpesya juu ya madhara makubwa ya mali na maisha ya watu
wakati wa ziara maalum ya kutoa pole kwa wahanga wa mvua iliyoandamana
na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa
mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa
Shinyanga.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa familia zilizoathirika na mvua
kali iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na
uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata,
Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akikagua baadhi ya makazi ya dharura kwa familia
zilizoathirika na mvua kali iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu
wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya
Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwapa mkono wa pole waalimu wa shule ya msingi
ya Mwakata, wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga, ambao pia ni waathirika
wa mvua kali iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya
watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya
Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia mamia ya wananchi baada ya kutembelea
na kuzifariji familia zilizoathirika na mvua kali iliyoandamana na mawe
na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali
katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa
Shinyanga. PICHA NA IKULU.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Machi 12, 2015, amefanya
ziara maalum ya kutoa pole kwa wahanga wa mvua iliyoandamana
na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu
mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya
Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
Rais Kikwete amewasili mjini Kahama kiasi cha saa nane
mchana baada ya ndege yake kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa
Mgodi wa Buzwagi na kwa muda wa kiasi cha saa tatu ametembelea
familia ambazo zimepata madhara makubwa zaidi kutokana na mvua
hiyo iliyonyesha kwa kiasi cha saa moja tu kuanzia saa nne usiku
Machi 3, mwaka huu, 2015 na kuambana na upepo mkali na mawe.
Watu 47 walipoteza maisha, 112 wakaumia, nyumba 657
zikabomolewa ama kuharibiwa na kaya 468 kuathirika katika vijiji
vitatu vya Kata ya Mwakata na tokea siku ya maafa, Serikali imetoa
huduma za dharura za chakula, sehemu za kulala, huduma za afya
na huduma nyingine muhimu kwa binadamu.
Baada ya kupatiwa maelezo ya kina na uongozi wa Mkoa wa
Shinyanga chini ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa
Ali N. Lufunga, Rais Kikwete ameanzia ziara yake katika Kijiji cha
Maghuhumwa, nyumbani kwa Bwana Masemba Maburi, ambaye
alipoteza watoto watano katika maafa hayo. Rais Kikwete ametoa
pole kwa wafiwa na kuzungumza na wananchi waliokuwepo kwenye
msiba.
Bwana Maburi ambaye sasa anaishi katika nyumba ya jirani
pamoja na familia yake na familia nyingine tatu amemweleza Rais
Kikwete jinsi nyumba mbili ambako watoto hao na mama yao
walipokuwa wamelala zilivyoanguka na mama huyo akalazimika
kukimbilia nje kwa nia ya kutafuta msaada lakini watoto wakazidiwa
na kupoteza maisha.
“Sijawahi kuona mvua kubwa, kali na yenye upepo mkali kiasi
kile katika maisha yangu. Mvua ilianza saa nne usiku na ikanyesha
kwa muda mfupi sana, nyumba zikaanguka ama kubomolewa.
Jameni tusaidie kwa sababu tumekwazika,”Bwana Maburi
amemwambia Rais Kikwete.
Baada ya kutoka katika Kijiji cha Maghuhumwa, Rais Kikwete
amekwenda katika Kijiji cha Nhumbi ambako amempa pole Bwana
Zacharia Limbe na familia yake ambayo ilipoteza wajukuu wanne
katika maafa hayo ya mwanzoni mwa mwezi huu.
Akiwa nyumbani kwa Bwana Limbe, Rais Kikwete ametembea
na kujionea makazi mapya ya dharura ya familia ambayo
yamejengwa kwa msaada wa Serikali.
Baada ya kuondoka kwa Bwana Limbe, Rais Kikwete
ametembelea eneo la makazi ya walimu wa Shule ya Msingi ya
Mwakata, ambako walimu hao wamehifadhiwa katika fremu za
maduka kutokana na athari za maafa hayo. Rais Kikwete amewapa
pole walimu hao na kuwaambia: “Pole sana. Tuko pamoja.
Tutaendelea kusaidiana kuona jinsi gani mnavyoweza kurejea katika
maeneo yenu ya makazi ya kawaida.”
Rais Kikwete ataondoka kesho, Ijumaa, Machi 13, 2015,
kurejea Dar es Salaam baada ya ziara hiyo maalum ya siku mbili
katika Mkoa wa Shinyanga.
No comments:
Post a Comment