Mhasibu
Mkuu wa Serikali,Mwanaidi Mtanda akiongea na waandishi wa habari jana
jijini Dar es salaam kuhusiana na mkutano wa 22 wa kimataifa wa Chama
cha Wahasibu Wakuu wa Serikali wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika
(ESAAG) utakaofanyika nchini kuanzia Machi 09, hadi 12 mwaka 2015.
Mwenyekiti
wa Kamati ya maandalizi ya mkutano wa 22 wa kimataifa wa Chama cha
Wahasibu Wakuu wa Serikali wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika
(ESAAG) ambaye pia ni Makamu Mhasibu Mkuu wa Serikali Azizi Kifile
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam
(hawapo pichani) kuhusu mkutano utakaofanyika nchini kuanzia Machi 09,
hadi 12 mwaka 2015.
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Tanzania
itakuwa mwenyeji wa mkutano wa 22 wa kimataifa wa Chama cha Wahasibu
Wakuu wa Serikali wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAG)
utakaofanyika nchini kuanzia Machi 09, hadi 12 mwaka 2015.
Kauli
hiyo imetolewa na Mhasibu Mkuu wa Serikali,Mwanaidi Mtanda kwa niaba ya
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile jana jijini Dar
es salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mkutano
huo utakaofanyika nchini.
Mhasibu
Mkuu wa Serikali Mwanaidi alisema kuwa mgeni rasmi katika mkutano huo
anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya
Kikwete.
Katika
mkutano huo, mada mbalimbali zinatarajiwa kujadiliwa zikilenga kwa
lengo la kukuza ushirikiano miongoni mwa nchi wanachama katika masuala
ya hesabu za serikali na kutoa fursa ya kuwa na jukwaa kwa ajili ya
washiriki ili kufanya tathmini kwa kujadiliana na kushirikishana uzoefu
mbali mbali.
Aidha,
mkutano huo unalenga kuhamasisha maendeleo ya watendaji wahasibu wa
Serikali na kutoa mafunzo stahiki kupitia utekelezaji wa program
shirikishi kwa kujifunza uzoefu wa masuala mbali mbali ndani ya nchi
wanachama.
Mkutano
wa wahasibu hao unatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 1000 wakiwemo
Wahasibu wakuu 14 kutoka nchi wanachama na wadau wengine.
Ujio
wa wageni hao pamoja na ushiriki wao katika mkutano wa siku tano utakuwa
wa tija na fursa muhimu katika utoaji wa huduma za jamii wakati wote
watakapokuwa nchini.
Aidha,
katika mahitaji yao ya malazi, chakula, usafiri na mahitaji mengine ya
msingi, makadirio ni kwamba kila mgeni anaweza kutumia zaidi ya shilingi
milioni moja, hivyo basi kwa hesabu za haraka haraka kutakuwa na
matumizi ya shilingi za kitanzania zaidi ya bilioni tano katika muda wa
siku tano tu.
“Wito
wangu kwa watanzania, nawaomba wajitokeze kushiriki katika mkutano huu
wa ESAAG wa 2015, hivyo natoa rai kwa wataalam, wahasibu na wadau wetu
wote kwa ujumla wao ili tuweze kushirikiana kuufanikisha mkutano huu wa
kimataifa unaofanyika nyumbani, Tanzania” alisema Mwanaidi.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mkutano huo ambaye pia
ni Makamu Mhasibu Mkuu wa Serikali Azizi Kifile amesema kuwa nchi
washiriki zinazounda umoja huo ni Botswana, Kenya, Lesotho, Malawi,
Mauritius, Msumbiji, Namibia, Rwanda, Afrika Kusini, Swaziland, Uganda,
Zambia, Zimbabwe na mwenyeji Tanzania.
Azizi
aliwahakikishia washiriki wote kuwa maandalizi ya mkutano huo katika
masuala ya usafiri, usalama na malazi yapo katika hatua nzuri na kamati
yake imejipanga vema ili mkutano huo uwe wa mfano wa kuigwa kwa nchi
zote wanachama watakapopata fursa ya kuandaa mkutano wa mwaka katika
nchi zao.
ni wa serikali wa nchi za mashariki na kusini mwa Afrika,Kwa bahati nzuri chama hiki kikiwa na malengo yafuatayo
ESAAG
ni chama cha wahasibu wakuu ambacho kilizaliwa miaka 20 iliypoita Arusha
hapa nchini mwaka 1995 na mkutano wa mwaka huu wa 22 wa ESAAG
unaongozwa na kauli mbiu “Uimarishaji na usimamizi wa fedha kwa ajili ya
Maendeleo ya kijamii na Kiuchumi katika kanda’’.
No comments:
Post a Comment