Mwili wa marehemu Nyaga paul Mawalla ukiwa katika kanisa la Kilutheri nchini Kenya usharika wa Uhuru Highway kwa ajili ya misa
****
Mazishi
ya Marehemu Nyaga Mawalla, aliyekuwa Mwasisi na Mkurugenzi wa Makampuni ya Mawalla
ya Jijini Arusha yamefanyika jana jijini Nairobi Kenya katia Makaburi ya Jumuia
ya Langata.
Mapema
kabla ya Mazishi hayo yaliyohudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali , familia na marafiki ilifanyika Misa ya kumuombea Marehemu katika Kanisa la
KKKK, Uhuru Highway.
Miongoni
mwa Viongozi waliohudhuria Mazishi hayo ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk.
Batilda Burian, Viongozi wastaafu, Sir. George Kahama, Mwemyekiti wa Chadema,
Freeman Mbowe, Wabunge, Mawaziri wanasheria mbalimbali wa ndani na nje ya
Tanzania.
Marehemu
Nyaga Paul Mawalla alifariki Machi 22, 2013 jijini Nairobi alikokuwa amelazwa
kwa matibabu zaidi.
Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini ,Chadema ni miongoni mwa waombolezaji waliokuwa kanisani nchini Kenya.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe,Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili
Lazaro Nyarandu na Sir George kahama wakiwa kanisani wakishiriki misa ya
maziko ya marehemu Nyaga Mawalla.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Batilda Buriani akiwa na mwanasheria
maarufu Jijini Arusha anayemiliki kampuni ya uwakili ya Law /Access
Advocates Mosses Mahuna wakiwa nje ya kanisa la Lutherani nchini Kenya.
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro wilani Simanjiro mkoani Manyara Christopher
Ole Sendeka na Waziri wa zamani wa mambo ya ndani Lawrence Marsha
wakiwa kanisani nchini Kenya maziko ya marehemu Paul Mawalla. Kwa picha na matukio zaidi bofya hapa >>>
No comments:
Post a Comment