Matukio: Push Mobile, UN na Wizara Kukabili EBOLA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Thursday, 26 February 2015

Matukio: Push Mobile, UN na Wizara Kukabili EBOLA

Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Push Mobile, Freddie Manento (kushoto) wakitiliana saini makubaliano ya ushirikiano wa kukabiliana na ugonjwa wa ebola kwa kutoa elimu kwa jamii kupitia ujumbe mfupi maneno katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za Mratibu mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa jijini Dar. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Dkt. Jama Gulaid.(Picha na Umoja wa Mataifa).

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya simu ya Push Mobile imetiliana saini na serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa (UN) ya kuwafikia watu milioni 10 ikiwahabarisha kuhusu ugonjwa hatari wa ebola.

Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa mjini hapa kampuni hiyo ya simu imesema kupitia ushirikiano huo kampuni hiyo ya simu itaunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa wa kutoa elimu dhidi ya ugonjwa huo ujumbe mfupi utakaoelezea ugonjwa wa ebola.

Kama sehemu ya makubaliano, Push Mobile , UN, serikali na wadau wake watatoa taarifa kuhusu ugonjwa huo wanapohitajika.

Watanzania wanaweza kupata habari za ugonjwa huo kwa kuandika neno EBOLA kwenye namba 15774 na kupata taarifa za ugonjwa huo bure bila kutozwa gharama.

Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez  na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Push Mobile, Freddie Manento wakionyesha hati za makubaliano ya ushirikiano huo.

 Wakitia saini Ofisa Mtendaji Mkuu wa Push Mobile, Freddie Manento amesema kwamba kama Ujumbe mfupi unaweza kuokoa maisha kampuni yake iko tayari kushiriki katika kampeni hiyo.

“..Teknolojia inatoa fursa ya pekee ya kuandaa jamii dhidi ya ugonjwa wa ebola na nini cha kufanya ukitokea. Kupitia ushirikiano huo kati yetu na Umoja wa Mataifa na Wizara ya afya na ustawi wa jamii tunaamini tutasaidia wananchi kuelekewa na kutambua dalili za ebola, kuzuia na kudhibiti maambukzi ya virusi vya ebola”, alisema Manento.

Katika miezi iliyopita vifo kutokana na ugonjwa wa ebola vimefikia 9000 huku vifo vingi vikitokea katika nchi za Liberia, Sierra Leone, na Guinea. Hadi sasa watu 23,000 wameelezwa kukumbwa na  ugonjwa.

Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Push Mobile, Freddie Manento kwa pamoja wakionyesha ujumbe mfupi wa maneno unaotoa elimu ya ugonjwa wa ebola kwa baadhi ya wageni waalikwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) waliohudhuria hafla hiyo.

Tanzania ikiwa na watumiaji wa simu milioni 30 na kufanya uwezekano wa kufikia watu hao kuwa ni asilimia 68.

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez  amesema teknolojia ya simu itasaidia sana kuleta uelewaq wa ugonjwa huo miongoni mwa Watanzania.

 “Mlipuko wa ugonjwa wa ebola  umepungua sana Afrika magharibi na  Tanzania haijawahi kukumbwa na ugonjwa huo.

 Lakini kunahitajika mtu mmoja tu kuwa na ugonjwa huo na kuleta mashaka makubwa katika maisha ya watu nchini. Tukiungana na sekta binafsi, Umoja wa mataifa unaunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii kuongeza upeo wa utayari katika kukabiliana na Ebola .”

Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Dkt. Jama Gulaid akimshukuru Ofisa Mtendaji Mkuu wa Push Mobile, Freddie Manento (kushoto) mara baada ya hafla fupi ya kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano huo. Kulia ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akishuhudia tukio hilo.

No comments:

Post a Comment