Na Mwandishi Wetu
Mkutano
uliowakutanisha Mawaziri wa nchi tano za Afrika Mashariki wakiwemo
Mabalozi wa nchini zao nchini Marekani ulifanyika Februari 25, 2015
katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, mkutano huo uliohusiana na
maandalizi ya kutiliana saini ya makubaliano ya ushirikiano wa
kibiashara na uwekezaji kati ya nchi ya Marekani na nchi za Afrika
Mashariki ambazo ni Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya na Tanzania.
Mkutano
huo uliongozwa na mwenyekiti wake Mhe. Harrison Mwakyembe Waziri wa
Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki pamoja na Katibu Mkuu wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Dkt. Richard Sezibera kutoka
Burundi.
Washiriki
wengine kwenye mkutano huo kutoka Tanzania walikua ni Waziri wa Viwanda
na Biashara wa Tanzania Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda, Waziri wa
Usafirishaji Mhe. Samwel Sitta, Maria Bilia Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Viwanda na Biashara, Amantius Msole, Naibu Katibu Mkuu MEAC Tanzania,
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula.
Washiriki
kwenye mkutano huo kutoka Burudi walikuwa ni Waziri wa Biashara na
Viwanda wa Burundi Mhe.Mzigiyimana Marie Rose, Balozi wa Burundi nchini
Marekani Mhe. Ndabashinze Ernest, Ntibarutaye Glorioje ambaye ni mshauri
ofisi ya Wizara ya Biashara ya Burundi,
Wawakilishi
kutoka Kenya walikuwa ni James Kiiru amabaye ni Mkurugenzi masaidizi
MFA & IT Kenya, Balozi Nelson Ndirangu ambaye ni mkurugenzi MFA
& IT Kenya, Bi. Phylus Kandie Cabinet Secretary MEACT Kenya, Ronnie
Gitonga Naibu Katibu Ubalozi wa Kenya nchini Marekani na Esther
Chemirmir PA to CS MEACT Kenya.
Wawakilishi
kutoka Uganda walikua ni Balozi wa Uganda nchini Marekani Mhe. Alfred
Nwam na Stilson Muhwezi. Rwanda waliwakilishwa na Waziri wa Bisahara
na Viwanda Mhe. Robert Opirah na Innocent Kabandana.
Mkutano
huo ni mwendelezo wa ule mkutano wa mwishoni mwa mwaka jana nchi ya
Marekani ilipowaalika Marais wa Afrika katika mkutano kama huo
ulioongozwa na Rais Barack Obama.
Waziri
wa Afrika Mashariki Mhe. Harrison Mwakyembe ambaye alikua mwenyekiti wa
mkutano wa kujiandaa kutiliana saini makubaliano ya biashara na
uwekezaji wa nchi za Afrika Mashariki na Marekani. Utiliano saini huo
utafanyika Februari 26, 2015 katika Ofisi za Wizara ya Biashara
Marekani, kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi
Dkt. Richard Sezibera kutoka Burundi.
Ujumbe wa Tanzania
Ujumbe wa Burundi
Ujumbe wa Kenya
Ujumbe wa Uganda na Rwanda
Mkutano ukiendelea.
Balozi
wa Tanzania nchini Martekani akiwa katika picha ya pamoja na Katibu
Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Richard Sezibera kutoka
Burundi.
No comments:
Post a Comment