Mwenyekiti
Mtendaji wa kampuni ya Forward Formidable Enterprises (FFE) inayoandaa
tamthilia mpya na ya kisasa ya “A boys mission” Johnson Lujwangana
katikati akifafanua jambo kuhusiana na tamthilia hiyo itakayoanza
kurushwa kwenye vituo vya televisheni kuanzia mwezi septemba. Wengine
katika picha kutoka kushoto ni Brian daniel, Neema Mung'anya, Samuel
katabazi, Jesca haule, Aisha bakari na Victor Casmir.
Mwenyekiti
Mtendaji wa kampuni ya Forward Formidable Enterprises (FFE) inayoandaa
tamthilia mpya na ya kisasa ya “A boys mission” Johnson Lujwangana
akifafanua jambo kuhusiana na tamthilia hiyo itakayoanza kurushwa kwenye
vituo vya televisheni kuanzia mwezi septemba. Wengine katika picha
kutoka kulia ni Jesca haule na Aisha bakari.
Waigizaji wa tamthilia ya “A boys mission” inayoandaliwa na kampuni ya Forward Formidable Enterprises katika picha ya pamoja.
Na Mwandishi wetu
Kampuni
mpya katika utengenezaji wa filamu nchini, Forward Formidable
Enterprises (FFE) inayoandaa tamthilia mpya na ya kisasa ya “A boys
mission” inahitaji kiasi cha Sh milioni 800 ili ikamilike.
Mwenyekiti
Mtendaji wa kampuni ya FFE, Johnson Lujwangana alisema kuwa kwa sasa
wameweza kutengeneza toleo la utangulizi "pilot episode' kwa ajili ya
kuonyesha nini wanakifanya huku kila kitu kikiwa tayari kwa ajili ya
kurekodiwa.
Johnson
alisema kuwa tamthilia yao inazungumzia changamoto na suluhisho
mbalimbali kwa maisha ya vijana nchini na fedha hizo zinahitajika kwa
ajili ya kughalimia gharama mbalimbali za kuzalisha rasmi tamthilia
hiyo.
Baadhi
ya gharama hizo kwa mujibu wa Johnson ni kulipa mtayarishaji bora,
kuwalipa wasanii fedha kutokana na ubora wa kazi zao, kulipia vifaa vya
kisasa, kulipa sehemu bora ya kurekodi tamthilia, usafiri, chakula na
gharama nyinginezo.
“Kama
msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond anatengeneza video ya dakika
tatu kwa Sh Milioni 60, kwa nini tamthilia ambayo kila sehemu (episode)
inatumia si chini ya dakika 45 hisifikia kiwango hicho cha fedha?
Alihoji Johnson.
Alisema
kuwa wao wanataka kuwafaidisha wasanii wao kwa kuwalipa vizuri na
kuendelea kudumu katika fani na kuwataka wadhamini kujitokeza kwa wingi
kusaidia mradi huo.
“Hakuna
hata msanii mmoja maarufu katika tamthilia hii, lengo si kama kuwatupa
wasanii hao, bali ni kupanua wigo na kuwapa nafasi wasanii wengine,
nataka kizazi kipya zaidi katika tasnia ili kuendeleza kuzalisha
mastaa,” alisema.
Alisema
kuwa katika tamthilia imeonyesha na kutoa majibu ya nini vijana
wanatakiwa kufanya hapa nchini na kuachana na fikra za kukimbilia nje ya
nchi kwa kudhani kuwa ndiko kutakuwa suluhisho la matatizo yao.
Alifafanua
kuwa mara baada ya kufika huko, hali inakuwa tofauti na kukutana na
changamoto nyingi zaidi za maisha na kuwaza kurejea nchini.
“Tamthilia
ni ya kisasa zaidi kwani lengo letu pia ni kuonyeshwa nje ya nchi na
kuonyesha madhari ya kuvutia ya jiji letu la Dar es Salaam na kupromoti
mji wetu tofauti na hali iliyozoeleka kwani tamthilia nyingi uonyesha
maisha ya vijijini,” alisema Johnson.
Alifafanua
kuwa kwa kuonyesha usafi wa mji, maeneo mbalimbali ya starehe ya hapa
nchini, kutawavutia hata wasanii watayarishaji wa tamthilia nje ya nchi
kuja kutayarishia kazi zao hapa nchini.
Alisema
kuwa tamthilia hiyo ina jumla ya sehemu 12 ambapo katika kila sehemu,
muigizaji mkuu ma maudhui ya tamthilia pia yanabadilika.
No comments:
Post a Comment