Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga (wa pili kutoka kulia)
akizungumza jambo na ujumbe kutoka Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Ujenzi
Dkt. John Magufuli. Ujumbe huo ulikwenda kumpa pole nyumbani kwake Bondo
nje kidogo ya mji wa Kisumu nchini Kenya kufuatia kifo cha mtoto wake
Fidelis Castro Odhiambo Odinga aliyefariki ghafla mapema mwezi huu.Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akimfariji mama mzazi wa
marehemu Fidelis Castro Odhiambo Odinga
Waziri
wa Ujenzi,Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mfiwa, Waziri Mkuu wa
zamani wa Kenya,Mh. Raila Odinga wakiongozana kuelekea sehemu maalum ya
kuaga mwili wa Marehemu Fidel Odinga kabwa ya kuzikwa kwake.
Waziri
wa Ujenzi,Dkt. John Pombe Magufuli akishiriki ibada ya kuaga mwili wa
Marehemu Fidel Odinga kabwa ya kuzikwa kwake.Kushoto ni Waziri Mkuu wa
zamani wa Kenya,Mh. Raila Odinga ambaye ni baba wa Marehemu.
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya,Mh. Raila Odinga ambaye ni baba wa Marehemu akimuombea mwanae.
Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Pombe Magufuli yupo nchini Kenya akiiwakilisha Tanzania kwenye mazishi ya mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya,Mh. Raila Odinga aitwaye Fidel Odinga aliefariki mwishoni mwa wiki iliyopita,yanayofanyika huko Bondo, Kisumu, Kenya.

No comments:
Post a Comment