Na Abdulaziz - Lindi
Mkuu wa mkoa wa Lindi,Mwantumu Mahiza ameitaka halmashauri ya wilaya
Ruangwa na halmashari nyingine za wilaya,miji,manispaa zilizopo mkoani
Lindi ambazo hazijachangia na zisizo kamilisha kuchangikia mifuko ya
vijana na wanawake zikamilishe kuchangia michango hiyo haraka.Mahiza
alitoa agizo hilo mjini Ruangwa baada ya kupokea taarifa ya kazi za
maendeleo katika wilaya hiyo iliyosomwa na kaimu mkuu wa wilaya
hiyo,Regina Chonjo.
Mahiza alisema halmashauri za wilaya zinawajibu wa
kuchingia mifuko hiyo kwa mujibu wa sheria badala ya kutafuta visingio
vinavyosababisha kutimizwa nia njema ya serikali kwa makundi hayo
maalum ya kijamii.Mkuu huyo wa mkoa ambaye yupo katika wilaya hiyo
kwa ziara ya siku mbili ili kukagua na kuhimiza utekelezaji wa mipango
mbalimbali ya maendeleo.
Alibanisha kuwa suala la halmashauri za wilaya
kutenga asilimia kumi ya mapato yake ya ndani ili kuchangia mifuko
hiyo siyo jambo la hiari bali ni lazima.Hivyo halmashauri hiyo na
nyingine zilizopo katika mkoa huu ambazo hazijachingia au
zisizokamilisha michango hiyo zikamilishe michongo yake haraka."
mnatakiwa mtambue kuwa vijana na wanawake kupewa fedha hizo siyo
zawadi bali ni haki yao,na ndiyo nia ya serikali wajiendeleze
kiuchumi," alisema Mahiza.
Awali akisoma taarifa hiyo kaimu mkuu wa
wilaya ya Ruangwa,Regina Chonjo alisema halmashauri ya wilaya ya
Ruangwa katika mwaka wa fedha 2014/2015 imechangia shilingi
20,000,000.00 kutoka katika mapato yake ya ndani yaliyokusanywa hadi
sasa,yenyejumla ya shilingi 946743451.72.
Ambapo katika kipindi
hicho(2014/2015) imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi
6000000.00,kwa vikundi 16 vya wanawake vyenye wanachama 80.Huku
ikiendelea kupokea maombi ya mikopo kutoka kwa vikundi mbali mbali vya
vijana na wanawake
Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Mh. Mwantumu Mahiza (wa pili kushoto) akiangalia
namna ya kushuka kwa usalama baada ya kukagua mradi wa Umwagiliaji
katika kijiji cha Chinokole wilayani Ruangwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya
Ruangwa,Ruebern Mfune akimsaidia kupanda Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea
ambae anakaimu wilaya ya Ruangwa,Mh. Regina Chonjo katika banio la umwagiliaji mara
baada ya mkuu wa mkoa kutembelea kukagua mradi huo utakaosaidia jamii
kwa kilimo cha umwagiliaji wilayani Ruangwa
Ujenzi ukiendelea katika jitihada za kuendeleza kituo cha umwagiliaji Chinokole wilayani Ruangwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Lindi,Mh. Mwantumu Mahiza akipata maelezo juu ya kusimama kwa
mradi wa ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ruangwa toka kwa Katibu
Tawala wa Mkoa wa Lindi Bw Abdallah Chikota na alie kushoto ni Kaimu
mkuu wa wilaya ya Ruangwa ambae pia ni Mkuu wa wilaya ya Nachingwea,Mh.
Regina Chonjo.
Baadhi ya madiwani,wakuu wa Idara katika Halmashauri
ya wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi wakisiliza Maagizo yaliyokwa
yakitolewa na mkuu wa mkoa wa Lindi,Mh. Mwantumu Mahiza(Hayupo
pichani)mara baada ya kumaliza ziara ya siku 2 wilayani humo kukagua
shughuli za maendeleo.
No comments:
Post a Comment