Mkuu
wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali (kushoto) akisalimiana na
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues
aliyemtembelea ofisini kwake wakati wa ziara ya kikazi ya siku nne
kwenye kijiji cha Ololosokwani na halmashauri ya Ngorongoro kwa ajili ya
maandalizi ya mradi wa kijiji cha digitali unaoendeshwa na Unesco kwa
kushirikiana na Ki-elektronic ya Samsung unaotarajiwa kuwasili kijijini
hapo mwezi februari ukitokea jijini Dar.
Na Zainul Mzige, Ngorongoro
MKURUGENZI
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues ameonesha mashaka yake
juu ya ubora wa barabara ambazo magari mazito yenye vifaa vya kijiji cha
digitali Ololosokwan yanaweza kupita.
Alisema hayo kwenye mazungumzo na Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Elias Wawa Lali wakati alipomtembelea ofisini kwake.
Akiwa
katika ofisi za mkuu huyo wa wilaya kumwelezea shughuli za Unesco
katika wilaya yake, Mkurugenzi Mkazi huyo alipata nafasi ya kuzungumzia
haja ya kuboreshwa kwa maaneo kadha ya barabara kuelekea kijiji cha
Olosokwan ili kuyawezesha magari hayo makubwa kufika kwa urahisi.
Huku
akimuonesha mkuu wa wilaya baadhi ya picha alizopiga akiwa njiani
kukagua njia ya kupita magari hayo na kuangalia maandalizi ya mwisho ya
mradi huo mkubwa na wa kipekee nchini alisema hali ya barabara si nzuri
hata kidogo.
Vifaa
kwa ajili ya kijiji hicho vipo bandarini tayari na magari yanayoweza
kubeba makontena hayo ni makubwa na barabara za kuelekea kijiji hicho ni
mbaya.
Mkuu
wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali (katikati) akizungumza na
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kulia)
aliyeambatana na wataalamu wa elimu, afya na mawasiliano pamoja na
Mratibu wa Taifa wa tiba asilia na mbadala katika Idara ya Tiba Wizara
ya Afya na ustawi wa jamii. Dkt Liggy Vumilia (hayupo pichani) . Kutoka
kushoto wa kwanza ni Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka
UNESCO, Bw. Herman Mathias, Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO,
Bi. Jennifer Kotta pamoja na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na
Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)
Bw. Al Amin Yusuph.
Kuwapo kwa kijiji hicho ni matokeo ya mkataba uliotiwa saini kati ya UNESCO na kampuni ya elektroniki ya Samsung mwaka jana.
Katika makubaliano hayo yalitiwa saini na Mwakilishi mkazi Unesco
nchini, Zulmira Rodrigues na Mkurugenzi wa Samsung Electronics nchini
Tanzania, Mike Seo katika Kijiji hicho kitakuwa na shule yenye Tehama
ikiwa na maunganisho ya intaneti, kiliniki ya kisasa ikiwa na kituo cha
teknolojia ya mawasiliano yenye kuwezesha utabibu (Telemedicine) na
jenereta linalotumia nguvu za jua kwa ajili ya kijiji hicho.
Mradi
huo utawezesha UNESCO kuwapatia vijana wa Kimasai elimu kutokana na
ukweli kuwa kwa utamaduni na kazi zao za ufugaji wamekuwa wakipata shida
ya kupata elimu.
Mkutano
huo pia ulihudhuriwa na wataalam wa Elimu, Afya, Utamaduni na Kilimo
kutoka Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro jijini Arusha. Kushoto
pichani ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Dkt. Peter Kitenyi.
Kupitia kijiji hicho vijana wataendelea na masomo hata kama wanachunga mifugo yao.
Wakati
wa utiaji saini Mkurugenzi wa Samsung Electronics nchini Tanzania
alitaja miongoni mwa manufaa makubwa yatakayopatikana katika mradi huo
wa kijiji cha digitali huko Loliondo ambayo ni pamoja na kuweza kupata
nishati rahisi na iliyo rafiki kwa mazingira.
Alisema
kwamba Afrika imekuwa mstari wa mbele katika uanzishaji wa vijiji vya
digitali. Aidha kwa kitendo hicho Afrika inaonesha dunia ni kwa namna
teknolojia inaweza kutumika kuleta mabadikliko chanya yanayotakiwa kwa
ajili ya maendeleo ya wananchi waliopo vijijini.
Kijiji
hicho cha Loliondo kitakuwa cha nne katika vijiji vya kidigitali barani
Afrika.Inatarajiwa kwamba kijiji kingine kitajengwa mjini Zanzibar kwa
ushirikiano wa UNESCO na Samsung Electronics mwaka huu.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akifafanua jambo kwa
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali wakati wa mazungumzo na
mkuu wa wilaya hiyo kabla ya kuelekea kijiji cha Ololosokwani kwa ajili
ya mkutano na wanakijiji wa kijiji hicho kabla ya kuwasili kwa mradi wa
kijiji cha kidigitali mapema mwezi februari.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akielezea changamoto
za miundo mbinu ya barabara kwa kutumia picha alizopiga akiwa njiani
kuelekea kijiji cha Ololosokwan kupitia barabara ya Lake Natron kwa Mkuu
wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali.
Mkuu
wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali akielezea jitihada
zitakazofanywa na wilaya yake katika kuhakikisha miundo mbinu ya
barabara inarekebishwa kuondoa usumbufu kwa magari mazito yenye vifaa
vya kijiji cha digitali cha Ololosokwan yanapita bila kikwazo mapema
mwezi februari.
Wataalamu
kutoka halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro, Unesco pamoja na Wizara ya
afya wakitazama picha hizo kwenye kompyuta mpakato ya Mkurugenzi Mkazi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues ofisini kwa Mkuu wa
wilaya ya Ngorongoro.
No comments:
Post a Comment