Wadigo wana msemo usemao " baraka hubarikiwa waliobarikiwa hata kama si majaaliwa" Naam, ukisikia Ngorongoro ni eneo pekee unaloweza kuona Wanyama wakubwa watano (The Big 5) si hadithi za kusadikika wala Ndoto za alinacha, ni dhahiri inayothibitishwa na nuru ya upeo wa macho yako
Fikiria unaingia tu getini, umbali wa nusu kilomita upande wako wa kushoto unashuhudia mti mkubwa umepambwa na mnyama adimu sana kuonekana nyakati za mchana, huyu si mwingine ni Anko Chui.
Sasa wakati Unamshangaa Chui inakulazimu ukimbizane na muda maana Big Five wengine kama Simba, Tembo, Faru na Nyati wanakusubiri Kasoko ya Ngorongoro wakiwa wamezungungukwa na makundi ya Pundamilia, swala, Pofu, viboko, Kasongo ndege aina Flamingo, Yangeyange, ndege karani na wengine wengi.
Ngorongoro ni hifadhi ya maajabu yenye Hadhi ya kimataifa, Destination ya maajabu, Bustani ya Eden, Nyayo za Laetoli, Tamaduni hai, Bonde la Olduvai na Mazalia ya Nyumbu.

No comments:
Post a Comment