UZINDUZI
wa kitabu cha msanii wa filamu hayati Steven Kanumba unatarajia
kuandika historia kufuatia maandalizi yaliyopangwa anasema mratibu wa
tamasha hilo Mohamed Mwikongi ‘Frank’ amesema kuwa kutakuwa na mambo
muhimu sana kwa ajili ya kumuenzi msanii huyo ambaye aliitangaza
Tanzania kimataifa.
“Tumepanga
kufanya mambo makubwa kwa ajili ya mwenzetu na tunataka ijengeke tabia
ya kuenzi wasanii mbalimbali, pesa za uzinduzi wa kitabu hiki utafungua
Kanumba Foundation kwa ajili ya kusaidia wanawake wajane na watoto
yatima,”anasema Frank.
Frank
anawakaribisha wadau wa Kanumba kwa kufika na kujione kazi za marehemu
Kanumba na kuoshuhudia wimbo maalumu wa Marehemu Kanumba utakaoimbwa na
mwanamuziki nyota Christian Bella kwa ajili ya tukio maalum .
Kitabu
cha historia ya maisha ya mwigizaji nyota Swahilihood Hayati Steven
Kanumba kinatarajiwa kuzinduliwa tarehe 10 January 2014 katika ukumbi wa
Landmark Ubungo, uzinduzi huo utaambatana na maonyesho ya kazi za
marehemu Kanumba alizowahi kushiriki na kuzifanya.
Mama
yake mzazi akiongea na waandishi wa habari amewashukru wale wote ambao
wamekuwa wakijaribu kufanya kazi ambazo kwa njia moja au nyingine
zinamkumbuka mwanaye ambaye aling’ara katika tasnia ya filamu
Swahilihood na kufanikiwa kutangaza Tanzania.
“Nawashukru
sana watanzania na wale ambao si Watanzania wamekuwa faraja sana
kwangu, hasa pale ambapo wamekuwa wakiona umuhimu wa kumuenzi Kanumba
kwa njia tofauti tofauti, nawashukru sana, na najua kila mtu ana mchango
mkubwa si rahisi kuwataja majina maana mpo wengi,”anasema mama Kanumba.
Kitabu
hiki kinachohusu maisha ya Kanumba The Great Fallen Tree kimeandikwa na
E. Emmanuel kutoka nchini Canada na kuhaririwa nchini Marekani na
kufanyiwa uchapishaji nchini Kenya.
Uzinduzi
wa kitabu utasindikizwa na Christian Bella na Bendi ya Malaika
kiingilio ni Ths. 20,000/ na utapata kitabu kimoja bure ukiingia tu
mlangoni na kazi zote za Hayati Kanumba zitapatikana siku hiyo. USIKOSE
TUKIO HILI LA AINA YAKE!
No comments:
Post a Comment