Mkuu
wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa
akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa
huduma ya BimaAFYA kati ya Vodacom Tanzania na Jubilee Insurance
itakayotolewa kupitia huduma ya M PESA, ambapo watanzania wenye kipato
cha chini watajiunga na huduma hiyo na kupata matibabu kwenye hospitali
zaidi ya 150 nchini. Ili kujiunga na huduma hiyo mteja anatakiwa kupiga
namba *150*57#. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Jubilee
Insurance, George Alande na Naibu Kamishina wa Bima Tanzania, Juma
Makame. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi
ya waandishi wa habari waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa huduma ya
BimaAFYA kati ya Vodacom Tanzania na Jubilee Insurance itakayotolewa
kupitia huduma ya M-PESA, ambapo Watanzania wenye kipato cha chini
watajiunga na huduma hiyo na kupata matibabu kwenye hospitali zaidi ya
150 nchini. Ili kujiunga na huduma hiyo mteja anatakiwa kupiga namba
*150*57#.
Naibu
Kamishina wa Bima Tanzania, Juma Makame (katikati) akishuhudia
Mkurugenzi Mkuu wa Jubilee Insurance, George Alande (kushoto) na Mkuu wa
Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzani,a Kelvin Twissa
wakipongezana baada ya uzinduzi wa huduma ya BimaAFYA kati ya kampuni
zao itakayotolewa kupitia huduma ya M-PESA, ambapo Watanzania wenye
kipato cha chini watajiunga na huduma hiyo na kupata matibabu kwenye
hospitali zaidi ya 150 nchini .Ili kujiunga na huduma hiyo mteja
anatakiwa kupiga namba *150*57#. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es
Salaam leo.
Naibu
Kamishina wa Bima Tanzania, Juma Makame (kulia) akioneshwa na Mkuu wa
Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa jinsi ya
kujiunga na huduma ya BimaAFYA wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo kati ya
Vodacom na Jubilee Insurance itakayowanufaisha wananchi wenye kipato
cha chini kupata matibabu kwenye hospitali zaidi ya 150. Huduma hiyo
itapatikana kupitia huduma ya M-PESA ili kujiunga na huduma hiyo mteja
anatakiwa kupiga namba *150*57#. Anaeshuhudia kushoto ni Mkurugenzi Mkuu
wa Jubilee Insurance, George Alande.
Hatimaye
sekta ya bima nchini imerahisisha huduma za bima ya afya kwa
kuwawezesha watanzania wenye kipato cha chini kujiunga na huduma mpya ya
bima ya afya iliyozinduliwa na kampuni ya Jubilee Insurance Tanzania
itakayotelwa kupitia huduma ya M-PESA.
Huduma
hii mpya ya BimaAfya ina unafuu mkubwa na inawalenga watu binafsi na
familia kwa ujumla na inamuwezesha atakayejiunga na huduma hii kupata
huduma za matibabu katika hospitali zaidi ya 150 nchi nzima –wenye
magonjwa ya kutibiwa mara moja,wagonjwa wenye magonjwa yanayopelekea
walazwe hospitalini na akina mama wajawazito watakaojiunga na huduma hii
watatibiwa bure!
Uchangiaji
wa kujiunga katika mfumo wa BimaAfya umerahisishwa ili kuwawezesha
wananchi kujiunga kulingana na vipato vyao,upo uchangiaji wa mwezi,mara
tatu kwa mwezi,nusu mwaka na mwaka mzima.
“Tanzania
kama zilivyo nchi nyingine za Afrika kwa muda mrefu haina utamaduni
unaowawezesha wananchi wake wote kuchangia na kufaidika na mfumo wa bima
ya afya zaidi ya wafanyakazi ambao wameajiriwa katika sekta rasmi na
hali hii inatokana na gharama za kuchangia bima ya afya kuwa kubwa kiasi
cha kuwashinda wenye vipato vya chini kuzimudu ambapo kuna idadi kubwa
ya watanzania wameachwa nje ya mfumo huu muhimu ambao ni muhimu kila mtu
kujiunga nao.BimaAfya itawawezesha watanzania kujiunga nayo kama
ambavyo wanapata huduma za kifedha kupitia huduma ya M-PESA” Anasema
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Kelivin
Twissa.
Kwa
upande wake Mtendaji Mkuu wa kampuni ya huduma za bima ya Jubilee
George Alande,amesema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 18 ya
watanzania ndio wanafaidika na huduma za bima ya afya nchini wengi wao
wakiwa ni waajiriwa.Kuna watu wachache wasio kwenye ajira ambao wanaweza
kulipia viwango vya bima za afya vilivyopo hivi sasa-hali inayopelekea
wananchi wengi waliojiajiri kwenye sekta isiyo rasmi kuachwa nje ya
mfumo huu wakiwemo wakulima,madereva wa daladala na wengineo wengi.
Pia
takwimu kutoka Mamlaka ya Usimamizaji wa Huduma za Bima nchini (TIRA) za
mwaka 2013 zinaonyesha kuwa waliokata bima za afya nchini ni asilimia
19% ya bima zote zilizokatwa.Hali hii inaonyesha kuwa kupitia huduma ya
BimaAfya iliyozinduliwa leo inapaswa kuchangamkiwa na watanzania wote
hususani wale wenye vipato vya chini.Ubunifu wa huduma hii kwa kiasi
kikubwa utawezesha kila mtanzania kupata huduma za bima kwa urahisi
kutoka kwa kampuni inayoongoza katika kutoa huduma za bima Afrika
Mashariki.
Naye
Mkurugenzi wa kampuni ya Edge Point ambayo pia ina ubia katika
ushirikiano huu wa kutoa huduma ya BimaAfya,Lilian Makoi amesema kuwa
matumizi ya teknolojia ni njia pekee ya kurahisisha huduma za kifedha
kwa watanzania wote wanaoishi mijini na vijijini na wenye vipato vya
aina mbalimbali ambao hapo awali ilikuwa ni vigumu kwao kupata huduma za
kifedha kama vile kujiunga na huduma za bima ya afya.
“BimaAfya
imebuniwa kuwapunguzia mzigo wa gharama za matibabu watanzania wenye
kipato cha chini hususani wale waliojiajiri katika sekta isiyo
rasmi.Huduma hii itawawezesha kupata huduma za matibabu katika hospitali
zaidi ya 150 nchini bila kulipa fedha taslimu.Malengo yetu ya baadaye
ni kusambaza huduma hii nchi nzima ili kuwawezesha wananchi wengi
kuchangia na kunufaika” alisema Ms Makoi.
Kujiunga
na huduma hii ya BimaAfya anachotakiwa kufanya mteja wa Vodacom ni
kupiga simu namba *150*57# na kutoa taarifa za awali
zinazotakiwa.Kinachofuatia ni kuchagua jinsi ya kufanya malipo kwa
kadri ya uwezo wake kupia huduma ya M-Pesa.Baada ya hapo atapata namba
ya utambulisho ya BimaAfya ambayo atakuwa anaitumia pindi atakapohitaji
kupata huduma kutoka hospitali zilizosajiliwa kutoa huduma hiyo.Kujiunga
na huduma hii ni kuanzia umri wa miaka 18 pia watoto wadogo wa wateja
waliojiunga watafaidika na huduma hii.Vigezo na masharti ya kujiunga
yanaelezwa wakati wa mchakato wa kujiunga.
No comments:
Post a Comment