Mbunge
wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akihutubia wananchi mjini
Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, Pwani, ambapo pamoja na kuwashuru kwa
kumchagua, pia alisema atatumia unasheria wake kuwasaidia wakazi wa
jimbo hilo wanaonyimwa haki zao za msingi ikiwemo kuporwa ardhi.
Ridhiwani akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo uliofanyika katika Uwanja wa Masoko mjini Chalinze
Mkazi
wa Chalinze, Bibi akitoa malalamiko yake mbele ya Mbunge Ridhiwani
Kikwete ya kudhulumiwa shamba lake na watu wasiojulikana.
Mkazi
wa Chalinze Methodius Kaijage, akiuliza swali kuhusu alama za x
zilizowekwa kwenye nyumba zao kwa ajili ya upanuzi wa barabara ambazo
alidai ni takribani miaka kumi imepita bila kupewa fidia hivyo
kusababisha kukosa maendeleo.
Sehemu ya wakazi wa Kata ya Bwilingu, wakiwa katika mkutano na mbunge wao mjini Chalinze.
Ridhiwani akihutubia wananchi katika Kitongoji cha Chalinze Mzee wakati wa ziara ya kuwashukuru wananchi na kusikiliza kero zao
Ridhiwani akimsalimia mmoja wa wazee wa Kitongozi cha Chalinze Mzee
Mmoja wa vijana wa Chalinze Mzee akiuliza swali
Mzee Ibrahim Koga akielezea mbele ya Mbunge asivyotendewa haki na Baraza la Kata ya Bwilingu la kuporwa ardhi yake
Mama
mwenye Jamii ya Kimasai Rehema Lazaro akilalamika mbele ya mbunge
kitendo cha baadhi ya wananchi kutoa lawama kwa wafugaji wote badala ya
wafugaji wanaofanya vurugu kwa kupeleka mifugo kwenye mashamba ya
wakulima na kuchafua visima vya maji.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
No comments:
Post a Comment