Gwiji
la Muziki wa Kizazi Kipya, Profesa J. akiwapagawisha mashabiki waliofika
katika Ufukwe wa Bahari Coco Beach kushuhudia Tamasha la Wazi
la”Vodacom Maisha ni Murua” lililofanyika jijini Dar es Salaam mahususi
kwa wateja wa kampuni hiyo katika kuukaribisha Mwaka 2015 jana.
Msanii
wa Muziki wa Kizazi Kipya, Roma Mkatoliki, akipanda jukwani
kuwaburudisha mashabiki wake waliofurika katika Ufukwe wa Bahari Coco
Beach kwenye Tamasha la Wazi la “Vodacom Maisha ni Murua”lililofanyika
jijini Dar es Salaam,Mahususi kwa wateja wa kampuni hiyo katika
kuukaribisha Mwaka 2015 jana.
Msanii
wa Muziki wa Kizazi Kipya, Roma Mkatoliki, akiwapagawisha mashabiki
wake waliofurika katika Ufukwe wa Bahari Coco Beach kwenye Tamasha la
Wazi la”Vodacom Maisha ni Murua”lililofanyika jijini Dar es
Salaam,Mahususi kwa wateja wa kampuni hiyo katika kuukaribisha Mwaka
2015 jana.
Baadhi
ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiwa wamefurika katika Ufukwe wa
Bahari Coco Beach kwenye Tamasha la Wazi la”Vodacom Maisha ni
Murua”lililofanyika jijini humo mahususi kwa wateja wa kampuni hiyo
katika kuakaribisha Mwaka 2015 jana.
Wanamuziki nguli wa muziki wa kizazi kipya wakiongozwa na Profesa J wamepagawisha mamia ya wapenzi wa muziki huo katika tamasha la wazi la kukaribisha mwaka mpya la”Vodacom maisha ni murua” lililofanyika katika ufukwe wa Coco beach jijini Dar es Salaam.Mbali na Profesa J,wanamuziki Temba,Mkatoliki nao walikonga nyonyo za washabiki.
Mwanamuziki wa kwanza kupanda jukwaani ambaye alipagawisha wapenzi wa muziki kisawasawa ni Profesa J,ambaye aliangusha vibao vyake vikali vinavyoendelea kutamba katika soko la muziki ndani na Nje ya nchi baadhi ya vibao vyake vikali vilivyowapagawisha mashabiki wake ni Zali la mentali wimbo huo aliemshirikisha Sir Nature,Kamiligado,ndiyo mzee na kumalizia na kibao cha hapo vipi ambacho kilipelekea mashabiki wake kulipuka na kuomuomba asishuke jukwaani aendelee kutoa burudani.
Aliposhuka jukwaani mwanamuziki Mheshimiwa Temba&Chege walipanda na kundi lake ambapo walikamua kisawasawa na kumwaga burudani iliyowafanya wapenzi wa muziki kucheza kwa furaha na kutamani asishuke jukwaani.
Aliyefunga pazia la kutoa burudani Mtoto wa kitanga Roma Mkatoliki naye alipagawisha wapenzi vilivyo kwa vibao vyake mbalimbali vikiwemo vipya na vya zamani.
Hadi mwisho wa tamasha wapenzi wengi walikuwa bado wanatamani lisiishe na baadhi yao walipohojiwa waliishukuru Vodacom Tanzania kwa kuwaandalia wateja wao tamasha hilo la burudani kemkem,Alisema Ramadhani Malenge mkazi wa Kawe jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu alisema kuwa Vodacom imeamua kuwaandalia wateja wake na wakazi wa jiji la Dar es Salaam tamasha hilo kwa ajili ya kuwapatia furaha na burudani wateja wake na wananchi kwa ujumla katika sikukuu ya mwaka mpya, vilevile wananchi walipata fursa ya kujinunulia bidhaa mbalimbali za Mawasiliano kwa gharama nafuu.
“Kama ilivyo kauli mbiu yetu kuwa “Ukiwa na Vodacom maisha ni murua”tunahakikisha mbali na kutoa huduma bora kwa wateja wetu pia tunajua kuwa kuna muda wanahitaji kufurahi kwa burudani hivyo ndio maana tunaandaa na kudhamini matamasha ya aina hii na tutaendelea kufanya hivyo siku zote ikiwa ni moja ya njia ya kusema ahsante kwa wateja wetu kwa kutuunga mkono”Alisema.
Alisema mwaka huu burudani kupitia matamasha haya imekuwa jijini Dar es salaam wakati mikakati inafanyika kuhakikisha burudani hii inasambazwa kwa wateja wote nchi nzima “Tunawajali na kuwasikiliza wateja wetu ambao kwetu ni wafalme hivyo tutahakikisha huduma bora na burudani katika kipindi maalum kama hiki inawafikia katika siku za usoni”.Alisema Nkurlu.

No comments:
Post a Comment