Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akiangalia baadhi ya
kazi zinazofanywa na wanavikundi wa UWAMAKI mara baada ya kuwasili
kwenye sherehe ya uzinduzi wa vikundi hivyo
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete akizindua
rasmi umoja wa vikundi vya wama katika Wilaya ya Kinondoni katika
sherehe ya kufana iliyofanyia kwenye Chuo cha Usafirishaji tarehe
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete akisoma
maandishi baada ya kuzindua rasmi umoja wa vikundi vya wama katika
Wilaya ya Kinondoni katika sherehe ya kufana iliyofanyia kwenye Chuo cha
Usafirishaji tarehe
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akijumuika na
wanavikundi vya UWAMAKI kusherehekea uzinduzi rasmi wa vikundi hivyo
huko Chuo Cha Usafirishaji.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akijumuika na
wanavikundi vya UWAMAKI kusherehekea uzinduzi rasmi wa vikundi hivyo
huko Chuo Cha Usafirishaji.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akijumuika na
wanavikundi vya UWAMAKI kusherehekea uzinduzi rasmi wa vikundi hivyo
huko Chuo Cha Usafirishaji.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake
mara baada ya kuzindua rasmi Umoja wa vikundi vya WAMA katika Wilaya ya
Kinondoni katika sherehe zilizofanyika katika Chuo Cha Usafirishaji
kilichoko eneo la Mabibo
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake
mara baada ya kuzindua rasmi Umoja wa vikundi vya WAMA katika Wilaya ya
Kinondoni katika sherehe zilizofanyika katika Chuo Cha Usafirishaji
kilichoko eneo la Mabibo
Baadhi
ya wanachama wa umoja wa vikundi vya WAMA katika wilaya ya Kinondoni
wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete wakati wa sherehe ya uzinduzi wa umoja wao
Baadhi
ya wanachama wa umoja wa vikundi vya WAMA katika wilaya ya Kinondoni
wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete wakati wa sherehe ya uzinduzi wa umoja wao
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipewa zawadi ya mkeka kutoka kwa wanachama
wa vikundi vya WAMA katika wilaya ya Kinondoni, UWAMAKI, WAKATI WA
SHEREHE ZA UZINDUZI WA Umoja wao
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama
Salma Kikwete akipeana mikono na Mwenyekiti wa Umoja wa vikundi
vinavyosimamiwa na WAMA katika wilaya ya Kinondoni (UWAMAKI), Ndugu
Christina Emmanuel wakati alipowasili kwenye Chuo cha Usafirishaji
kilichoko eneo la Ubungo kwa ajili ya ufunguzi wa umoja huo. Picha na
John Lukuwi
Na Anna Nkinda – Maelezo
Vijana
wametakiwa kujiunga na vikundi vya kuweka akiba na kukopa ili
kuchangia mawazo yao na ubunifu na wakati huo huo wanajitengenezea
mazingira ya kujiajiri kwani wengi wao wana elimu na ujuzi
walioupata masomoni lakini wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira.
Rai
hiyo imetolewa leo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akizindua
Umoja wa Vikundi vya kuweka Akiba vilivyopo chini ya Taasisi ya Wanawake
na Maendeleo (WAMA) wilaya ya Kinondoni (UWAMAKI) katika ukumbi wa
mikutano wa chuo cha Usafirishaji jijini Dar es Salaam.
Mama
Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA alisema kupitia
vikundi hivyo vijana wanaweza kupata mitaji midogomidogo pamoja na
mafunzo ya kuwawezesha kuanzisha biashara na kujiajiri. Kwani mfumo huo
wa vikundi na mafunzo ni moja ya njia za kuwajengea vijana uwezo wa
kujiajiri na hivyo kupunguza tatizo la ajira.
Kwa
upande wa wanachama wa UWAMAKI aliwasisitiza kutoridhika na mafanikio
waliyoyapata bali waendelee kutafuta njia za kupiga hatua hususani
kupata utaalamu wa kuboresha bidhaa zao , kutafuta masoko zaidi na
kufanya ubunifu wa kuweza kuvumbua bidhaa na biashara nyingine tofauti
ili kuepukana na ushindani wa soko.
“Mnapokuwa
na bidhaa zinazofanana mtakuwa katika mazingira ya kushindania soko
jambo ambalo litapunguza kiasi cha mauzo ambayo ndiyo pato lenu
wajasiriamali. Jitihada ifanywe ili kuweza kutafuta watalaam ambao
watawapa mafunzo ya kukuza biashara”, alisema Mama Kikwete.
Akisoma
risala ya vikundi hivyo Katibu wa UWAMAKI , Mwajuma Waziri aliishukuru
Taasisi ya WAMA kwa kuwawezesha kuwa na vikundi na kupata mafunzo ya
kuweka akiba, elimu ya kibenki, usindikaji wa vyakula na huduma ya bima
ya afya.
Waziri
alisema, “Kutokana na mafunzo hayo tunaweza kuanzisha miradi mbalimbali
kama vile kutengeneza sabuni za maji za kufulia, sabuni za kuoshea
vyombo na kusafishia tairizi, siagi ya karanga na batiki na hatimaye
tumeweza kufungua akaunti yetu ya Umoja katika benki ya wanawake (TWB)”.
Katibu
huyo alisema walianza na kikundi kimoja kwa kujiwekea hisa moja kwa
thamani ya shilingi 1000 pia waliweza kukopesha kiasi cha shilingi
6,300,000 mpaka mwisho wa mwaka walivuna shilingi 12,750,000.
“Hadi
sasa tunavikundi 11 vyenye wanachama 274 kati ya hao wanaume ni wanane
katika vikundi hivi tumeweza kukopesha kiasi cha shilingi 47,500,000/=
na kufikia mavuno ya shilingi 79,739,000 kwa mwaka”, alisema.
Alimalizia
kwa kusema lengo la kuunda umoja huo ni kushirikiana katika matatizo ya
kijamii, kuunda SACCOS na kutafuta masoko ya bidhaa zao.
Taasisi
ya WAMA inasimamia mradi wa kuwawezesha wanawake kwa kuwapa mafunzo
kupitia vikundi katika mikoa ya Dar es Salaam Lindi na Pwani hadi
kufikia Septemba mwaka huu jumla ya watu 18,000 wamefikiwa kwa kupitia
vikundi 688 vilivyoundwa na tayari shilingi milioni 227 zimekusanywa na
kukopeshwa.
No comments:
Post a Comment