Meneja
wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera, Bw. Ashwin Rana akiwakaribisha wageni
kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipotembelea kiwanda hicho
ikiwa ni sehemu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo nchini. Anayesalimiana
naye ni Prof. Longinus Rutasitara (Naibu Katibu Mtendaji Uchumi Jumla).
Katikati ni Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri.
Timu
ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
ikikagua mitambo ya kuzalishia sukari katika Kiwanda cha Sukari cha
Kagera.
Kiongozi
wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Bibi Florence Mwanri (Mwenye kofia ya bluu) akionja sukari
inayozalishwa na Kiwanda cha Sukari cha Kagera. Kushoto ni Mratibu wa
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Bw. Senya Tuni.
Timu
ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Kiwanda cha Sukari cha
Kagera. Nyuma ni shehena ya sukari iliyo tayari kuingia sokoni.
Timu
ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
wakioneshwa mashine ya kumwagilia maji miwa ijulikanayo kwa kitaalamu
kama Centre Pivot System.
Meneja
wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera, Bw. Ashwin Rana (Kulia) akiwaonesha
Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
mashine mpya zinazotumika kuvutia maji kwa ajili ya kumwagilia miwa.
Msimamizi
Mkuu wa Mtambo wa maji wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera, Mhandisi Abdul
Adinani (Kulia) akitoa maelekezo ya namna ya maji yanavyochujwa kabla
ya kutumika kwa ajili ya umwagiliaji wa miwa. Wanaomsikiliza ni Wakaguzi
wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Mtaalamu
wa uchongaji na usawazishaji wa ardhi kwa ajili ya mashamba ya miwa,
Mhandisi Ali Khamis (Kulia) akitoa maelezo ya namna matrekta yanayotumia
setalaiti (hayapo pichani) yanavyofanya kazi. Wanaomskiliza ni Prof.
Longinus Rutasitara (Kushoto) ambaye ni Naibu Katibu Mtendaji
anayeshughilikia masuala ya Uchumi Jumla na Katikati ni Kiongozi wa
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Bibi Florence Mwanri.
Timu
ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
wakioneshwa kwa vitendo matrekta yanayotumia setalaiti kusawazisha
shamba kwa ajili ya uzalishaji miwa.
PICHA NA SAIDI MKABAKULI
Na Saidi Mkabakuli, Kagera
Kiwanja
cha Sukari cha Kagera kimeanza kuzalisha ziada ya sukari inayohitajika
katika soko la sukari nchini hali inayopelekea kuweza kupunguza tatizo
la upatikanaji wa sukari Tanzania na nchi za jirani zinazotumia sukari
kutoka kiwandani hapo.
Hayo
yamewekwa wazi na Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho, Bw. Ashwin Rana, wakati
alipokuwa akizungumza na Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
“Kwa
sasa tumeweza kuongeza mauzo katika kanda kufikia tani 40,000, pamoja na
kuongeza ununuzi kutoka kwa wakulima wa miwa wa nje zaidi ya tani
100,000 kwa mwaka,” alisema.
Bw.
Rana aliongeza kuwa Kiwanda chake kimewekeza zaidi katika upanuzi wa
eneo la shamba la miwa la umwagiliaji la hekta 3600 pamoja na kuwekeza
zaidi katika teknolojia ya kisasa katika kilimo.
“Kampuni
yetu imewekeza kwa kiasi kikubwa katika teknolojia na vifaa vya kisasa
ikiwemo matrekta yanayotumia setalaiti katika ufanyaji kazi wake katika
kuandaa mashamba,” aliongeza.
Kiongozi
wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Bibi Florence Mwanri amekipongeza Kiwanda hicho kwa kuwekeza
kwenye uzalishaji wa kisasa wa miwa hali inayoongeza uzalishaji wa
sukari kuwa mkubwa kiwandani hapo.
Bibi
Mwanri ameongeza kuwa Kiwanda hicho kinastahili pongezi za kipekee kwa
kuweza kuongeza ajira zaidi ya watu 6000 waliopo kiwandani.
“Kwa kweli munastahili sifa kwa kutoa ajira kwa vijana wa Kitanzania pamoja na kuuza umeme kwenye gridi ya Taifa,” alisema.
Kwa
mujibu wa Meneja wa Kiwanda hicho, kwa sasa kinakabiliwa na na
changamoto za uuzaji haramu wa sukari zinazoingia kimagendo nchini ambao
umechangiwa kushindwa kwa kiwanda kuuza sukari ili kurudisha gharama za
uzalishaji kutokana bei za sukari zinazoagiwa kutoka nje kuwa bei ya
chini sana.
“Bei
ya Sukari Duniani imeshuka sana kutokana na Nchi kubwa duniani kusaidia
wakulima katika uzalishaji na pembejeo (subsidies) na hivyo sukari
kuuzwa katika soko la dunia kwa bei ya chini (Dumping) na kufanya kuwa
bei kuwa ndogo kuliko gharama halisi ya uzalishaji,” aliongeza.
Aliongeza
kuwa changamoto nyingine ni pamoja na kiwanda kushindwa kulipa mikopo
iliyochokuwa benki kutokana na kuwepo sokoni kwa sukari ambayo ni ya
magendo na bei ya chini hivyo kiwanda kushindwa kufikia malengo hata ya
kiundeshaji na mipango mikakati.
Kiwanda
cha Sukari cha Kagera kiko katika sehemu Kaskazini Magharibi ya
Tanzania (karibu na mpaka wa Tanzania na Uganda) kilibinafsishwa na
Serikali kwa sekta binafsi mwaka 2001.
Malengo
ya ubinafsishaji yalikuwa kuboresha upanuzi wa masoko ya ndani na
kikanda, uwekezaji wa kisasa, upanuzi na ukarabati na majengo ili
kuhakikisha shughuli za kiundeshaji zinaboreshwa.
No comments:
Post a Comment