Desemba 16 mwaka huu Waziri wa Mambo ya nje ya Nchi ,Mh Benard Membe alikabidhi bendera kwa Balozi Adadi Rajabu kwa niaba ya Mabalozi ,ikiwa ni ishara ya kuanzisha safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro na safari hiyo ilianza kwa muda wa siku sita. |
Safari ilianza kwa taratibu huku Mabalozi wakitizama mandhari tofauti ya uoto wa asili katika Mlima Kilimanjaro. |
Safari ya kuelekea Kileleni hivi ndivyo ilivyoendelea kuchukua kasi kwa Mabalozi . |
Waziri wa mambo ya nje ya nchi ,Mh Benard Membe akioneshwa moja ya kibao kilichokuwa kikielekeza muelekeo wakati wa kupanda Mlima Kilimanjaro. |
Waziri wa mambo ya nje ya nchi ,Mh Benard Membe akipita katika moja ya daraja kuelekea eneo la Nusu njia. |
Baada ya kuongoza msafara wa Mabalozi kama ishara ya kuanzisha upandaji wa mlima Kilimanjaro kwa Mabalozi,hatimaye Waziri wa mambo ya nje ya nchi ,Mh Benard Membe alifika eneo la Nusu njia. |
Waziri wa mambo ya nje ya nchi,Mh Benard Membe akipata chakula na mkuu wa wilaya ya Rombo ,Elenas Parangyo mara baada ya kufika katika eneo la Nusu Njia(Kisambioni) |
Wageni waliokuwa wakipanda Mlima Kilimanjaro walipata nafasi ya kupiga picha na Waziri wa mambo ya nje ya Nchi,Benard Membe. |
Mabalozi wakiwa na Waziri wa mambo ya nje ya nchi,Benard Membe wakipata chakula katika eneo la Nusu Njia. |
Mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja eneo la Kisambioni. |
Mabalozi wakiwa katia picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya nje ya nchi ,Benard Membe katika eneo la Kisambioni ,eneo ambalo mh Membe aliwaaga Mabalozi katika safari yao ya kupanda Mlima Kilimanjaro. |
Baada ya kupumzika katika eneo la Kisambioni na kupata chakula ,safari iliendelea ya kwenda kituo cha Mandara. |
Kila mmoja alikuwa na Morali ya juu wakati wote wa kupanda Mlima Kilimanjaro. |
Wakati mwingine Mabalozi walilazimika kupumzika na kupoza koo kabla ya kuendelea na safari . |
Baada ya mapumziko safari ya kupanda Mlima iliiendelea . |
Wasaidizi katika kupanda Mlima Kilimanjaro kutokana na uzoefu walionao ,wao walifika mapema katika kituo cha Mandara kwa ajili ya Maandalizi . |
Baada ya safari ya takribani saa tano hatimaye ujumbe wa Mabalozi uliwasili kituo cha kwanza cha Mandara. |
Mabalozi baada ya kufika katika kituo cha kwanza cha Mandara walipata fursa ya kuchukua taswira mbalimbali kwa ajili ya kumbukumbu. |
Baada ya safari ndefu ya kutoka Lango la Marangu ambako ni mwanzo wa safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro ,Mabalozi walipata chakula cha usiku na kisha kupumzika kwa ajili ya maandalizi ya siku inayofuata ya kuelekea kituo cha Horombo. |
Globu ya Jamii ikiwakilishwa na mwakilishi wake kanda ya kaskazini Dixon Busagaga ilishiriki katika safari hiyo ya Mabalozi kupanda Mlima Kilimanjaro ,Tegemea kupata taarifa za matukio yote tangu kuanza kwa safari hiyo hadi kilele cha Mlima Kilimanjaro kupitia hapa hapa Globu ya jamii. |
No comments:
Post a Comment