Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Desemba 26, 2014
kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ya kuwaaga jumla ya watoto
55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, waliofadhiliwa na
Lions Club ya jijini, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto
hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo.
Rais
wa Lions (Host) Club ya Dar es Salaam, Mathew Levi, akizungumza wakati
wa hafla fupi ya kuwaaga watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo
kati ya 104, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa
awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo.
Baadhi ya wadau waliohudhuria hafla hiyo.
Badhi ya watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, wakiwa na mama zao wakati wa hafla hiyo.
Badhi ya watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, wakiwa na mama zao wakati wa hafla hiyo.
Badhi ya watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, wakiwa na mama zao wakati wa hafla hiyo.
Badhi ya watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, wakiwa na mama zao wakati wa hafla hiyo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiteta jambo na Rais wa Lions (Host) Club ya Dar es Salaam, Mathew
Levi, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto 55 wenye matatizo ya
ugonjwa wa Moyo kati ya 104, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India.
Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akivishwa Beji ya miaka 50 ya Lions Club na Makamu wa Gavana wa Club
hiyo, kwa nchi za Tanzania na Uganda, Hyderali Gangji, wakati wa hafla
fupi ya kuwaaga watoto wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo wanaokwenda
nchini India kutibiwa. Hafla hiyo ilifanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye
Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi zawadi mtoto, Nabil Hahya (4) kutoka Jijini Dar es Salaam,
mmoja kati ya watoto 55 wa awamu ya kwanza kati ya 104 wenye matatizo ya
ugonjwa wa Moyo wanaokwenda kutibiwa nchini India, wakati wa hafla fupi
ya kuwaaga watoto hao iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli
ya Serena Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mama wa motto huyo, Amina
Yahya.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi zawadi mtoto, Hyria Ally (miezi 9) Kutoka Zanzibar, mmoja
kati ya watoto 55 wa awamu ya kwanza kati ya 104 wenye matatizo ya
ugonjwa wa Moyo wanaokwenda kutibiwa nchini India, wakati wa hafla fupi
ya kuwaaga watoto hao iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya
Serena Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mama wa motto huyo, Zulekha
Said.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na mmoja kati ya watoto wanaokwenda kutibiwa nchini India,
wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa ya
moyo iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na baadhi ya wadau wa Lions Club, baada ya hafla fupi ya
kuwaaga watoto hao. Picha na OMR
No comments:
Post a Comment