Mkuu
wa Bandari ya Kigoma, Bw. Athuman Malibamba (Kulia) akimkaribisha
Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) mara alipofika kujionea
maendeleo ya bandari hiyo.
Sehemu ya chelezo zinazotumika kwa ajili ya matengenezo ya meli na boti katika Bandari ya Kigoma.
Mkuu
wa Bandari ya Kigoma, Bw. Athuman Malibamba (Katikati mbele) akifafanua
jambo kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango mara walipofika kujionea shughuli za maendeleo kiwanjani
hapo.
Kiongozi
wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Bibi Florence Mwanri (Aliyenyanyua mkono) akionesha kufurahia
jambo wakati walipofanya ziara katika Bandari ya Kigoma.
Mkuu
wa Bandari ya Kigoma, Bw. Athuman Malibamba (Wapili kulia) akifafanua
jambo kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango mara walipofika kujionea shughuli za maendeleo kiwanjani
hapo.
Boti na meli zikipandisha shehena kwenye Bandari ya Kigoma.
PICHA ZOTE NA SAIDI MKABAKULI
Serikali
imeazimia kuendelea kuboresha miundombinu ya bandari hususan miradi
iliyoibuliwa katika Programu ya Matokeo Makubwa Sasa ikiwemo kuanza
kufanya upanuzi wa Bandari ya Kigoma na kuendelea kuboresha miundombinu
na ununuzi wa vifaa mbalimbali vya kuhudumia shehena katika Bandari ya
Kigoma ili kuweza kukidhi mahitaji yanaongeza siku baada ya siku katika
bandari hiyo.
Ahadi
hiyo imetolewa na Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo
kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati
walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miundombinu katika Bandari ya
Kigoma.
Bibi
Mwanri alisema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Bandari nchini nchini
ipo kwenye mkakati wa kuiendeleza bandari hiyo ili iwe ya kiwango kizuri
kwa kuhudumia watumiaji wa wa bandari hiyo.
“Kama
munavyokumbuka Serikali katika mwaka huu wa fedha ilipanga kuiendeleza
na kuboresha miundombinu ya usafiri wa majini na anga ili kuongeza
ufanisi wa sekta hizi, ambapo Bandari ya Kigoma ni mojawapo ya bandari
zilizopewa kipaumbele kwa ajili ya uendelezaji,” alisema Bibi Mwanri.
Kwa
mujibu wa Bibi Mwanri, upanuzi wa bandari hiyo upo kwenye hatua za
upembuzi yakinifu kwa ajili ya kuboresha bandari ya Kigoma na kutwaa
maeneo zaidi kwa ajili ya upanuzi wa bandari hiyo.
Akitoa
taarifa ya maendeleo ya Bandari hiyo, Mkuu wa Bandari hiyo Bw. Athuman
Malibamba alisema kuwa mpaka kufikia Juni 2014 hatua ya utekelezaji
iliyofikiwa ni kukamilika kwa kazi ya uthamini wa mali eneo la Kibirizi
lenye hekta 10 kwa ajili ya upanuzi wa bandari hiyo. “Pia, Mamlaka
imempata Mtaalam Mshauri (M/S Royal Haskoning H.D.V Nederland, B.V)
atakaefanya kazi ya Upembuzi Yakinifu. Aidha, kazi ya uthamini wa mali
imekamilika kwa eneo la Katosho lenye hekta 69 kwa ajili ya kujenga
bandari kavu,” alisema.
Kuongezeka
kwa shughuli za kiuchumi katika nchi za jirani kunatoa fursa ya
kuimarisha miundombinu ya bandari ya Kigoma ili kuwa na uwezo wa
kuhudumia shehena inayoongezeka na kukuza uchumi katika mkoa na Taifa
kwa ujumla. Aidha kuanzishwa kwa Eneo Maalum la Kiuchumi, katika mkoa wa
Kigoma ni kichocheo muhimu kwa Mamlaka ya Bandari (TPA) kuimarisha
huduma katika bandari ya Kigoma na hivyo kuweza kuzitumia fursa
zitakazojitokeza mara baada ya shughuli mbalimbali za kiuchumi
kuanzishwa.
No comments:
Post a Comment