Waziri Nyalandu akiwa na watoto wake wakati wa ibada maalum
iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Ilongelo Jimbo la
Singida Kaskazini
Nyalandu na Faraja Kota wakiwa na watoto wao Sera na Christopher katika kanisa hilo
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu
akitoa neno la shukrani baada ya ibada maalum katika katisa la KKKT
Usharika wa Ilongelo jimboni humo
Waumini wakiwa katika kanisa la FPCT wakati wa ibada maalum aliyohudhuria Nyalandu
Nyalandu
na Mkewe wakitoka katika Kanisa la FPCT baada ya kuhudhuria ibada
maalum asubuhi. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu
akizungumza na viongozi wa shule ya Kiislam ambayo huhudumia watoto wa
dini zote katika kata ya Ilongelo, shule hiyo ina watoto 74.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akisalimia waumini kwenye Kanisa
la FPCT katika jimbo la Ilongelo alipofika kwa ajili ya ibada maalum
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo
Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota
kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa
Ilongelo, jimboni humo
Steve
Nyerere ambaye ni Msanii na Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM,
akizungumza kabla ya kumwaga vimbwanga vyake vya kuingiza sauti za
viongozi mbalimbali wakati wa mkutano huo wa Nyalandu.
Mwanamuziki wa muizki wa Injili, Rose Muhando akiimba kutumbuiza wananchi katika mkutano huo wa Nyalandu
Wadau wakifurahia burudani wakati wa mkutano huo wa Nyalandu
Wasanii wa kikundi cha Makomandoo cha mjini Singida wakitumuiza wakati wa mkutano huo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo
Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota
kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa
Ilongelo, jimboni humo.Picha na Bashir Nkromo
----
WAZIRI wa maliasili na utalii na mbunge wa jimbo la Singida
kaskazini(CCM) ,Lazaro Samwel Nyalandu,ametangaza rasmi nia ya kugombea
nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Nyalandu ametangaza nia hiyo leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Ilongero Jimbo la Singida kaskazini.
Alisema baada ya kutafakari kwa muda mrefu na
kujikagua kwa kina,ameona anao uwezo wa kutosha wa kuweza kupokea kijiti
kutoka kwa rais anayemaliza muda wake mwakani kwa mujibu wa katiba.
“Kujikagua huko ni pamoja na kutafakari jinsi
alivyoweza kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM katika vipindi vitatu
(miaka 15) akiwa mbunge wa jimbo la Singida kaskazini.Katika kipindi
hicho cha ubunge,nimeweza kutumia zaidi ya shilingi bilioni mbili katika
kufanikisha kuchangia miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali
zikiwemo za afya,maji na barabara”,alisema Nyalandu.
Alisema wakati ukifika,Watanzania kutoka sehemu
mbalimbali za nchi wakiongozwa na wakazi wengi wa kutoka jimbo la
Singida kaskazini,kwenda Dodoma kuchukua fomu za kuwania urais.
“Watanzania waliokwisha onyesha nia ya kuwania
urais mwakani,nawaomba sote tuonyeshe kazi tulizozifanya katika
kuwahudumia Watanzania,ili waweze kutupima vizuri waweze kujijengea
mazingira mazuri ya kuchangua rais atakayewafaa kwa kuwaletea maendeleo
endelevu”,alisema.
Nyalandu alisema kuwa anakishukuru Chama Cha
Mapinduzi,kwa maandalizi yake mazuri ya kuhakikisha chama kinapata
mwanaCCM safi,mwadilifu na mchapa kazi atakayepeperusha bendera ya chama
katika kinyang’anyiro cha kuwania urais mwakani.
No comments:
Post a Comment