Mwenyekiti
wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Zuhura Songambele
(kulia), akionesha katiba ya chama hicho wakati akizungumza na waandishi
wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu chama hicho kupata viongozi wapya
na mambo mengine. Kushoto ni Katibu wa TAPSEA, Festo Melkiory.
Makamu Mwenyekiti wa TAPSEA, Janejelly James (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti
wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Zuhura Songambele
(katikati) akiwa na viongozi wenzake, Kutoka kulia ni Mjumbe wa chama
hicho, Godfrey Ngoloka, Makamu Mwenyekiti, Janejelly James, Katibu wa TAPSEA, Festo Melkiory na Marcelina Mshumbusi (Mjumbe).
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Dotto Mwaibale
UONGOZI
mpya wa Chama cha Makatibu Mahsusi (TAPSEA), umejipanga kutatua kero na
matatizo mbalimbali yanayo wakumba makatibu mahsusi nchini.
Akizungumza
Dar es Salaam wakati akitambulisha uongozi wa awamu ya pili wa chama
hicho ambao ulichaguliwa Julai mwaka huu, Mwenyekiti wa chama hicho
Taifa, Zuhura Songambele alisema uongozi huo mpya pia umejipanga
kuhakikisha utekelezwaji wa sera ya ajira, fedha na utawala unafanyiwa
kazi.
Alisema
katika juhudi za kutatua kero hizo pia watahakikisha wanatokomeza
unyanyasaji wa jinsia mbao umekuwa kero kwa makatibu mahususi wakiwa
sehemu zao za kazi.
Songambele
alitaja majina ya uongozi huo ni Zuhura Songambele, ambaye ni
mwenyekiti, Makamu mwenyekiti Janejelly James, Katibu Festo Elikiory,
Naibu katibu Rose Mwalimu.
Alitaja
majina mengine ambayo ni ya wajumbe Monica Bayuni, Marcelina
Mashumbusi, Catherine Mshatta, Atupakisye Mapuli, Vicky Eben, Godfrey
Ngoloka, Fatma Kahungenge, Beatrice Mwasumbwi na Rose Kasiga.
Aliwataka
makatibu mahsusi kujiunga na chama hicho ilikuweza kuwasilisha
malalamiko yao na kuwa na sauti moja katika jamii na kuweza kuchukua
hatua mbalimbali zitakazo wasaidia.
Alisema
kuna zaidi ya makatibu 4000 nchini hivyo aliwataka waajiri kuwashawishi
makatibu hao kujiunga na chama hicho ili kufanikisha mambo mbalimbali
ya makatibu mahsusi.
No comments:
Post a Comment