
Chama Cha Riadha kilikaa kikao tarehe 6 December 2014 mjini Dar Es Salaam, kikao hicho kilichoelezewa kuwa kikali kuwahi kupata kutokea katika hitoria ya chama hicho kilimweka Katibu wa RT Suleiman Nyambui kiti moto hadi akafanya jaribio la kutaka kukimbia ukumbini.
Baada ya shutuma nyingi, zote zikielekezwa kwa Nyambui na
wajumbe wote wa RT hatimaye mzee akakiri huku akitetemeka kwamba:
- -
Alipokea hongo ya Tsh: 500,000 kutoka kwa
wanariadha waliokwenda mazoezi kambi za nje.
- -
Ndiyo maana hakuruhusu utaratibu wa mchujo
kwanza ili awapange wale waliokubali kumlipa.
- -
Pia amekiri kuendesha semina zisizotambuliwa na
RT na kuguhi sahihi zilizopo kwenye vyeti.
- -Amekiri yote hayo baada ya baadhi ya wajumbe
kutishia kuweka wazi ushahidi walionao.
KUMBUKUMBU:
Watanzania wakumbuke kwamba kupitia blog hii tumeshawahi kumtahadharisha Waziri
Membe kuwa makini na fedha za walipa kodi. Sasa unaona mhehimiwa Waziri? Fedha
ulizotoa kwa moyo wa kizalendo imekuwa chanzo cha ufisadi wa ndani ya RT!
Pia Nyambui alikaririwa na chombo kimoja maarufu cha habari
hapa nchini mwezi July mwaka huu akikiri kwamba “Aliwahi kuwasafirisha watu
ambao walibainika kubeba madawa ya kulevya hadi Australia” Je Nyambui anaendelea
kufanya nini RT?
Chanzo : www.gidabuday.blogspot.com
No comments:
Post a Comment