Kesi
ya kuchoma moto bendera ya CCM inayomkabili Mbunge wa Arumeru Mashariki
(Chadema), Joshua Nassari (pichani) jana iliahirishwa na Ofisa Mtendaji
wa Kata ya Maji ya Chai, Ndikilo Mbise kutokana na Hakimu wa Mahakama
ya Mwanzo ya Maji ya Chai, David Mwita kuwa safarini.
Akiahirisha
kesi hiyo, Mbise alisema itatajwa tena Januari 20 mwakani.Mbise alisema
Hakimu Mwita amepata msiba, hivyo amekwenda nyumbani kwao mkoani Mara
huku, hakimu mwingine wa mahakama hiyo akiwa likizo.
Mbise alisema ameahirisha kesi na kuipangia tarehe nyingine kwa kuwa ni mlinzi wa amani wa eneo hio.
Katika
kesi hiyo, Nassari ambaye hakuhudhuria mahakamani hapo kutokana na kuwa
safarini, anatuhumiwa kuchoma bendera ya CCM Desemba 15, saa 11 jioni
katika eneo la Maji ya Chai. Bendera hiyo yenye thamani ya Sh250,000
ilikuwa mali ya Raphael Moses.
Ilielezwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa ataendelea kuwa nje kwa dhamana ya wadhamini watatu ya Sh1.5 milioni kila mmoja.
Chanzo : Mwananchi
No comments:
Post a Comment