Kiongozi
wa idara ya utalii Arusha Bi.Anita Temba akiongea na washiriki wa
shindano la Model of Tourism Tanzania mara baada ya kufanya ziara yao
katika makao makuu ya TANAPA jijini Arusha ambapo waliweza kufahamu
shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika hilo
Meneja
Mahusiano wa TANAPA Pascal Shelutete akizungumza na washiriki wa
shindano la Model of Tourism Tanzania mara baada ya kufanya ziara yao
katika makao makuu ya TANAPA jijini Arusha
Kiongozi wa idara ya utalii Arusha Bi.Anita Temba akiteta jambo na mratibu wa shindano hilo Samdia Charles
Mkurugenzi
mkuu hifadhi za Taifa ,Tanzania Allan Kijazi akiwa katika picha ya
pamoja na washiriki wa shindano la Model of Tourism Tanzania mara baada
ya kufanya ziara yao katika makao makuu ya TANAPA jijini Arusha
Mkurugenzi
wa utalii na masoko Ibrahim Mussa akiwa anawasikiliza washiriki wa
shindano la Model of Tourism Tanzania mara baada ya kufanya ziara yao
katika makao makuu ya TANAPA jijini Arusha (hawapo pichani)ambapo
aliwataka washiriki hao kutumia nafasi hiyo kutangaza utalii wa ndani
Mkurugenzi mkuu hifadhi za Taifa ,Tanzania Allan Kijazi akipata utambulisho kutoka kwa washiriki wa shindano hilo
Washiriki wakipata picha ya pamoja nje ya jengo la makao makuu ya TANAPA jijini Arusha
Kiongozi wa idara ya utalii Arusha Bi.Anita Temba akiwa anatoa maelekezo kwa washiriki wa shindano la Model of Tourism Tanzania
Na Pamela Mollel wa jamiiblog
Washiriki
wa shindano la Model of Tourism Tanzania wametakiwa kutumia fursa hiyo
katika kutangaza utalii wa ndani hali itakayopelekea idadi kubwa ya
watanzania kutembelea hifadhi za Taifa
Rai
hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa utalii na masoko Ibrahim Mussa ,jana
wakati washiriki wa shindano hilo walipopata fursa ya kutembelea makao
makuu ya TANAPA jijini Arusha
Bw.
Mussa aliwataka washiriki hao kutumia fursa hiyo katika kutangaza utalii
wa ndani hali itakayo pelekea idadi ya watanzania kujitokeza kwa wingi
kutembelea hifadhi za Taifa
Alisema
kuwa ipo haja kwa watanzania kuona utalii ni sehemu ya starehe ambayo
unaweza kujifunza hata ukiwa na familia yako tofauti na starehe zingine
Naye
Maratibu wa shindano hilo Samdia Charles alisema lengo la kuanzishwa kwa
shindano hilo ni kuhamasisha utalii wa ndani na kutangaza vivutio vya
nchi yetu kimataifa kupitia maonyesho ya mavazai kama vile new York
fashion week,Paris fashion week na Victoria’s secret fashion show
Aidha alisema kuwa katika shindano hilo washiriki wametoka katika mikoa mbalimbali ya Dar es saam, Arusha,Iringa,Mbeya,Manyara, Singida,Kilimanjaro,Tanga, Tabora,Dodoma na Mwanza
Shindano hilo lilianzishwa mwaka 2013 ambapo mwaka huu kuna jumla ya
washiriki 19 kati yao 16 ni mabalozi wa hifadhi za taifa na shindano
hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 22 novemba 2014katika ukumbi wa
triple A jijini Arusha
No comments:
Post a Comment