Mwenyekiti
na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of
Industries), Alhaji Aliko Dangote (kulia) mfanyabiashara maarufu kutoka
Nigeria, akiteremka kwenye ndege alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa
Mtwara, kwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda kikubwa cha saruji
kinachojengwa mkoani humo.
Dangote akilakiwa na Mwakilishi Mkazi wa kampuni hiyo nchini, Esther Baruti (kushoto)
Dangote akisalimiana na Balozi Mdogo wa Nigeria nchini, Adamu Mussa
Dangote
akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa kampuni ya Dangote nchini, Esther
Baruti na Balozi Mdogo wa Nigeria nchini, Adamu Mussa
Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries),
Alhaji Aliko Dangote (kulia) mfanyabiashara maarufu kutoka Nigeria,
akilakiwa na Mwakilishi Mkazi wa kampuni hiyo nchini, Esther Baruti
(katikati) pamoja na Balozi Mdogo wa Nigeria nchini, Adamu Mussa
alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho, mkoani
Mtwara
Balozi Mdogo wa Nigeria, Adamu Mussa akizungumza na Dangote Uwanja wa Ndege wa Mtwara
Dangote
akisalimiana na wafanyakazi wa kampuni inayojenga kiwanda hicho ya Dil
& Sinoma, baada ya kuwasili eneo la ujenzi wa kiwanda.
Dangote akiwa katika kikao na baadhi ya wahandisi na mafundi wa wanaojenga kiwanda hicho
Alhaji Aliko Dangote akitabasamu baada ya kuwasili eneo la ujenzi wa kiwanda hicho
Dangote akitumia gari kukagua ujenzi wa kiwanda hicho
Mwenyekiti
na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of
Industries), Alhaji Aliko Dangote akiwa kwenye gari huku akipata maelezo
ya ujenzi wa kiwanda hicho kutoka kwa mafundi na wahandisi ya Dil &
Sinoma inayojenga kiwanda hicho kitakachokuwa cha tatu kwa ukubwa
Afrika.
Msafara
wa Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote
Groupof Industries), Alhaji Aliko Dangote, ukikagua ujenzi wa kiwanda
hicho kinachotarajiwakuanza kazi Aprili, mwakani. Awamu ya kwanza ya
kiwanda hicho ujenzi wake ukikamilika kitakuwa kinazalisha tani 6000 kwa
siku.
Dangote akiangalia moja ya majengo yanayoendelea kujengwa kiwandani hapo
Mwenyekiti
na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of
Industries), Alhaji Aliko Dangote (kulia) mfanyabiashara maarufu kutoka
Nigeria, akizungumza na Meneja Mkuu wa Kiwanda kikubwa cha cha saruji
cha Dangote Tanzania, Daljit Singh (katikati), alipotembelea na kukagua
maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho,mkoani Mtwara. Kushoto ni Kenneth
Kasigila ambaye ni Msaidizi Maalumu wa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB,
iliyopewa fursa ya kwanza kujenga benki karibu na kiwanda hicho.PICHA
ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
No comments:
Post a Comment