Mratibu
wa mradi wa kudhibiti wanyama wakali kwa kutumia waya na
mitii maalumu inayohimili ukame unaofadhiliwa na UNDP Dr. Maurus
Msuha akitoa maelezo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa
na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez (kulia) alipotembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa
na shirika la UNDP wilayani Longido mkoani Arusha katika ziara
yake ya siku mbili mara baada ya kuwasili wilayani humo. Katikati
ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania
Hoyce Temu aliyeambatana na Mwakilishi huyo.
Na Mwandishi wetu,
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez,
amewataka wadau wa mazingira nchini kuwasaidia wananchi wa
vijijini hasa wafugaji kutumia nguvu na rasilimali walizonazo
kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi kwa
kuendelea kuhifadhi mazingira na viumbe vilivyopo wakiwemo
wanyamapori
Bw,
Rodriguez aliyasema hayo wilayani Longido mkoani Arusha katika
ziara yake ya siku mbili ya kutembelea baadhi ya miradi
inayofadhiliwa na shirika hilo .
Akizungumza
baada ya kutembelea na kuzindua mradi wa kuwawezesha wafugaji
wa wilaya ya Longido kupunguza ukataji wa miti kwa ajili ya
kujenga uzio wa kulinda mifugo yao na wanyama wakali Bw,
Rodriguez, amesema kutokana na uelewa mdogo wa mabadiliko
yanayoendelea kutokea wananchi wengi wa vijijini wanahitaji
msaada wa namna ya kuyadhibiti.
Mratibu
wa mradi wa kudhibiti wanyama wakali kwa kutumia waya na mitii
maalumu inayohimili ukame unaofadhiliwa na UNDP Dr. Maurus Msuha
akiendelea kutoa maelezo kwa Mwakilishi huyo Bw. Alvaro Rodriguez
(katikati), wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Longido Mheshimiwa James
Ole Millya.
Aidha
alisema kwa sasa wananchi wengi wanatumia muda na nguvu nyingi
kushughulikia matokeo ya athari za mabadiliko ya tabia ya nchi
na maeneo mengi wamekuwa wakijikuta wanagombana wenyewe kwa
wenyewe badala ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya msingi.
"mara
nyingi wananchi wa vijijini kama hawa wafugaji mmekuwa
wamekuwa wakilaumiwa kwa matokeo ya yale wanayoyafanya kwa
kusukumwa na mabadiliko haya na mengine wangeweza kuyajua wala
wasingeyafanya "alisema Rodriguez.
Aidha
Bw. Rodriguez ambaye pia ni Mkuu wa miradi ya maendeleo
inayofadhiliwa na shirika hilo hapa nchini amewataka viongozi
na watendaji wakiwemo watalaam kutumia muda na uwezo wao
kuwasaidia wananchi wa vijijini hasa wafugaji na kwamba UNDP
itaongeza nguvu kusaidia makundi hayo.
Mratibu
wa mradi wa kudhibiti wanyama wakali kwa kutumia waya na mitii
maalumu inayohimili ukame unaofadhiliwa na UNDP Dr. Maurus Msuha
akimwoonyesha eneo maalum lililowekwa uzio kwa ajili ya kulinda mifugo
na wanyama wa kali Mwakilishi huyo Bw. Alvaro Rodriguez aliyefika wilani
hapo kukagua miradi hiyo.
Mratibu
wa mradi wa kudhibiti wanyama wakali kwa kutumia waya na
mitii maalumu inayohimili ukame unaofadhiliwa na UNDP Dr. Maurus
Msuha ambaye pia ni mtafiti mkuu wa wanyama katika taasisi ya
utafiti wa wanyamapori TAWIRI amesema mradi huo umeonyesha
mafanikio makubwa kwa kuanza kupunguza uhasama kati ya wafugaji
na wanyama pori wanaokula mifugo yao wakiwemo Simba na Fisi.
Kwa
upande wao viongozi na wananchi akiwemo Mkuu wa wilaya ya Longido
Bw James Ole Milya wamesema pamoja na changamoto
zinazowakabili wanaendelea kutilia mkazo suala la utunzaji wa
mazingira na wanyamapori kwani licha ya kuwa ni asili yao
ndio msingi wa maisha yao.
Mkuu
wa Wilaya ya Longido Mheshimiwa James Ole Millya (kulia) akifafanua
jambo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez (wa pili kushoto) wakati alipotembelea wilaya hiyo kukagua
maendelo ya miradi inayofadhiliwa na shirika la UNDP. Kushoto ni
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez
akisalimiana na na wanawake wa kimasai mara baada ya kuwasili wilayani
Longido kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika la UNDP.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mkuu wa
Wilaya ya Longido Mheshimiwa James Ole Millya kwa pamoja wakizundua
uzio wa kuhifadhia mifugo ya jamii ya wafugaji wilayani Longido wakati
alipokuwa kwenye ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na shirika la
UNDP.
Muonekano wa uzio utakaotumika kuhifadhia wanyama wasidhurike na wanyama wakali mara baada ya kuzinduliwa rasmi.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akitoa
nasaha zake kwa jamii ya wafugaji wa wilaya ya Longido mkoani Arusha
alipofanya ziara ya siku mbili kukagua miradi inayofadhiliwa na shirika
la UNDP.
Baadhi
ya wakazi wa Longido ambao shughuli zao kubwa ni ufugaji
wakimsikiliza Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez (hayupo pichani).
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akivishwa
zawadi ya shuka la kimasai na mmoja wa wafugaji wa wilaya hiyo.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez,
akisikiliza maelezo ya zawadi za asali za Nyuki wadogo na wakubwa
kutoka kwa jamii za wafugaji wanaofadhiliwa na shirika la UNDP wakati
alipofanya ziara ya kukagua miradi hiyo wilayani humo.
No comments:
Post a Comment