
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof.
Elisante Ole Gabriel akipokea Cheti cha heshima kutoka kwa Muwakilishi
wa Mfuko wa PSPF,Abdul Njaidi ambao ni sehemu ya Wadhamini wa Bendi hiyo
ikiwa ni sehemu ya heshima kwa Mh. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa
mchango wake mkubwa kwa wasanii mbali mbali hapa nchini.Cheti hicho
kimetolewa na Bendi ya Msondo Ngoma.

Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof.
Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimkabidhi Cheti cha heshima mpiga solo
hodari wa Bendi ya Msondo Ngoma,Abdul Ridhwan "Panga mawe"

Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof.
Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimkabidhi Cheti pamoja fedha taslim sh.
Mil. 5,Hassan Moshi William (mtoto wa Marehemu TX Moshi Willian) kwa
niaba ya baba yake.

Mtangazaji
Mkongwe hapa nchini na mwenye historia na Muziki wa Tanzania,Masoud
Masoud (kulia) akionyesha moja ya CD za bendi ya Msondo Ngoma zilizokuwa
zikinadiwa kwenye sherehe hizo mbele ya Wadhamini.
Safu
ya waimbaji wa Bendi ya Msondo Ngoma ikiongozwa na Nguli Shaaban Dede
(katikati) wakifanya vitu vya mbele ya mashabiki wao lukuki waliofika
kwenye Viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar.

Rapa wa Bendi ya Msondo Ngoma,Roman Mng'ande akifanya mambo.

Baba la Mababa,Mzee Said Mabela akiendeendelea kuzikonga nyoyo za Mashabiki wa Msondo.

Abdul Ridhwan "Panga mawe". Picha Zote na Othman Michuzi.
No comments:
Post a Comment