Waombolezaji wakiwa na jeneza la msanii Mabovu kutoka msikiti wa Mwangata kwenda makaburi ya Mlolo Iringa |
Msafara wa magari kwenda kumzika mabovu |
Waombolezaji wakiuzika mwili wa Mabovu |
WEUSI wakiwa katika mazishi ya mabovu |
Bashiri akiongelea kifo cha Mabovu |
Watangazaji wa Radio Ebony Fm waliofika katika mazishi hayo leo |
Msanii Nurdin kushoto akiwa na Geofrey Ngelime wakati wa mazishi ya Mabovu |
Wadau wa Mabovu wakiwa katika picha mara baada ya mazishi mwenye nguo nyekundi ni mtangazaji wa Ebony Fm Edo Bashiri , wa tatu kulia ni msanii DJ Nacy na msanii Nurdin |
Marafiki na wasanii mbali mbali wakiweka chata zao katika kaburi ya Mabovu |
Baadhi ya wasanii wa kundi la Weusi ambao wamefika Iringa kumzika msanii Mabovu |
Picha na habari na kikosi cha matukiodaima.co.tz
Vituko vyatawala msiba wa msanii Ahmed Zubery Upete a. k. a Geez Mabovu Iringa mlevi (pichani aliyekaa chini)atembeza kichapo kwa wafiwa kisa ataka aruhusiwe kuufukua mwili wa marehemu ili auage Mara ya mwisho asisitiza kuwa marehemu amekua nae na ana siri nzito ya kifo chake.
Tukio hilo limetokea muda mfupi baada ya mwili wa marehemu kuwasili makaburi ya Mlolo nje kidogo ya mji wa Iringa kwa mazishi.
Chapombe huyo ambae alifika makaburini hapo kwa kuchelewa alivamia eneo hilo la mazishi kwa kuanza kutoa lugha za matusi ya nguoni kwa wafiwa kwa madai wamewezaje kumzika marehemu huyo bila ya yeye
kufika eneo hilo.
Kutokana na lugha hizo za matusi iliwalazimu Vijana waombolezaji kumtoa kwa nguvu eneo hilo na kwenda nae pembeni kidogo kumsihi asifanye vurugu kabla ya chapombe huyo kuanza kurusha Ngumi kwa wasanii.
Akizungumza
mara baada ya mazishi hayo mmoja kati ya wadau wa tasinia ya
muziki nchini na promota mkubwa wa mziki nyanda za juu kusini Edwin
Bashir ambae ni mtangazaji wa kituo cha Radio Ebony Fm alisema
kuwa mbali ya umoja ambao wasanii wameuonyesha katika msiba huo kwa
kuja kushiriki mazishi ila bado angeshauri wasanii kwa wakati
mwingine kujenga ushirikiano wa kumjulia hali mwenzao pindi anapoumwa.
"
Sisemi kwa ubaya ila kiukweli msanii Geez Mabovu ameumwa sana
karibu mwaka mzima anasumbuliwa na ugonjwa wake ila hakuna msanii
ambae amefika kumjulia hali ila leo wengi wamesafiri kuja
kumzika..... inapendeza kusaidiana wakati wa ugonjwa badala ya
kusubiri mwenzenu afe "
Bashir
alisema kuwa msanii huyo ni miongoni mwa wasanii wa mwanzo zaidi
kuutangaza mkoa wa Iriga katika tasnia ya muziki na kuwa hata kabla ya
vituo vya radio kuanzishwa mkoani Iringa alikuwa akiutangaza mkoa na
kusikika katika radio mbali mbali za nje ya Iringa.
Alisema
kuwa msanii huyo toka amemaliza elimu yake kamwe hajapata kufanya
shughuli nyingine nje ya mziki na kuwa wakati wote alikuwa
akijishughulisha na muziki zaidi .
Hata
hivyo alisema chanzo cha Mabovu kuhama mkoa wa Iringa na kuhamishia
makazi yake jijini Dar es Salaam ni kuzidi kuutangaza muziki zaidi
na mkoa wake wa Iringa malengo ambayo alipata kufanikiwa kwa kiasi
kikubwa .
"
Utaona jinsi ambavyo msiba wake ulivyowavuta watu wegi
wapenzi na wadau wa muziki kutoka mikoa mbali mbali ya nje ya Iringa
ambao kimsingi baadhi yao imekuwa ni mara yao ya kwanza kufika Iringa
....pamoja na kufarijika kwa umati wa watu waliofika kumzika ila
moyo umeniuma sana hasa ukizingatia kuwa kifo chake hakikuwa na
ghafla bali amekufa kwa mateso makubwa kwa kuugua karibu mwaka
mzima sasa hivyo kwa umoja huo ningetegemea wangefika enzi za uhai
wake kumuuguza mwenzao"
Kwa
upande wake mwakilishi kwa kundi la Weusi Bw Joh Makini alisema
kuwa kifo cha Mabovu kimeacha pengo kubwa katika tasnia ya muziki
hasa muziki wa hiphop Tanzania,
Alisema
kuwa Mabovu amepata kuishinae Kinondoni Jijini Dar es Salaam mtaa
mmoja ila pia amepata kushirikiana kazi mbali mbali za kimzuki .
Hivyo
alisema kuwa ushirikiano huo ndio ambao umewasukuma kufika mkoani
Iringa kushiriki mazishi hayo baada ya pengo kubwa ambalo
wamelipata .
Akizungumza kwa niaba ya wasanii wazawa na mkoa wa Iringa msanii Squza,alisema
kuwa Iringa imempoteza msanii mkongwe na kuwa kifo chake
kitaenziwa na wasanii wa mkoa wa Iringa pia ambao wapo nje ya mkoa
huo kwa kuangalia jambo la kufanya katika kuwanyanyua wasanii
chipukizi wa mkoa huo.
Alisema
kuwa wapo wasanii maarufu wengi kutoka mkoa wa Iringa ambao wana
majina makubwa kama Rehema Chalamila (RAY C} akina MiKe T na
wengine wengi na kuwa kama njia ya kumuenzi Mabovu watahakikisha
wanaunganisha nguvu kwa kushirikiana na vyombo vya habari kuona
Iringa inampata mwakilishi mwingine wa Mabovu kutoka kwa wasanii
Chipukizi .
No comments:
Post a Comment