Mazishi Kesho :Mwili wa Marehemu Robert Lengeju Waagwa Jijini Dar Kuzikwa Kesho Kipera Morogoro. - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 12 November 2014

Mazishi Kesho :Mwili wa Marehemu Robert Lengeju Waagwa Jijini Dar Kuzikwa Kesho Kipera Morogoro.


Hili ndilo sanuku lililouhifadhi mwili wa Mwandishi/Mchambuzi wa Jukwaa Maalumu la MWALE WA DEMOKRASIA katika Gazeti la Raia Tanzania (Gazeti dada la Raia Mwema), kila Alhamisi. Mwili wa shujaa huyo wa Demokrasia uliswaliwa katika Kanisa Katoliki M<simbazi Jijini Dar es Salaam leo. 

Watu mbalimbali walihudhuria katika misa hiyo ya kumsindikiza Lengeju katika safari yake ya mwisho kabla ya maziko yatakayo fanyika kesho (Novemba 13,2014) Kijijini kwako Kipera, Kata na Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro. Na Mroki Mroki-Father Kidevu Blog.
 Ndugu wa marehemu Robert Lengeju wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mdogo wao.
Heshima za mwisho ziliendelea kutolewa na ndugu jamaa na marafiki.
Godfrey Dililunga kutoka kampuni ya Raia Mwema wachapaji wa gazeti la Raia Mwema na Raia Tanzania akitoa heshima za mwandishi huyo wa Makala za Mwale wa Demokrasia katika gazeti lao.
Mhariri wa Raia Mwema, Ezekiel Kamwaga akitoa heshima kwa mwili wa marehemu.
Waombolezaji wakipita kutoka heshima za mwisho.
Mkuu wa Mkoa wa Mstaafu, Isdore Shirima nae alikuwepo kutoa heshima za mwisho kwa Lengeju.
Waombolezaji
wanakwaya wakiimba katika misa hiyo.
wanafamilia wakiwa Kanisani katika misa.
Wanafamilia, ndugu jamaa na marafiki wakiwa katika misa hiyo leo.
 Kaka wa Marehemu Charles Lengeju akiwa amebeba msalaba wa marehemu.
Gari lililobeba mwili wa marehemu Robert Lengeju likiwa tayari kwa safari ya Kipera Mkoani Morogoro.

No comments:

Post a Comment