Afya Zetu : Dkt. Seif Rashid Azindua Kongamano la Tisa la NHIF na Waandishi wa Habari Mkoani Dodoma - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Friday, 14 November 2014

Afya Zetu : Dkt. Seif Rashid Azindua Kongamano la Tisa la NHIF na Waandishi wa Habari Mkoani Dodoma


Pichani ni Mgeni rasmi Waziri wa Afya,Dkt.Seif Rashid akizungumza wakati wa kuzindua kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa Habari,lililofanyika katika moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani humo,ambapo kauli mbiu ya kongamano hilo ni ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,Bwa.Hamisi Mdee  akizungumza katika kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa Habari,lililofanyika katika moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani humo,ambapo kauli mbiu ya kongamano hilo ni ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.Kabla ya uzinduzi wa kongamano hilo Wanahabari walishiriki kutembelea miradi mbalimbali ya afya,ikiwemo hopsitali ya Mkoa wa Dodoma pamoja na Kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya binadamu kilichopo ndani ya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),ambacho imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 36 zilizotolewa na NHIF,kituo hicho kinatarajiwa kuanza kazi rasmi mapema mwakani.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF,Bwa.Raphael Mwamoto akifafanua jambo kwenye kongamano la tisa la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), na Waandishi wa habari lililofanyika katika moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani humo,ambapo kauli mbiu ya Kongamano hilo ni ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya kutoka wilaya mbalimbali walioko mezani mbele wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye kongamano hilo la tisa la NHIF,ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Afya,Mh.Dkt Seif Rashid ndiye aliyezindua kongamano hilo lililohudhuriwa na Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali,
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,Bwa.Hamisi Mdee na pichani kati ni Mgeni rasmi Waziri wa Afya,Mh.Dkt Seif Rashid wakifuatilia na kusikiliza kwa makini baadhi ya maswali na changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiulizwa na washiriki wa Kongamano hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba,Mh.Yahya Nawanda akizungumza mbele ya washiriki wa kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari kuhusiana na mmpango mzima wa wananchi wake kutumia bima ya Afya,na pia alifafanua kuhusiana na mikakati mbalimbali anayotumia kuwahamasisha wananchi wake katika suala zima la kuhakikisha kila mtu anakua Bima ya Afya.
Pichani ni baadhi ya Wadau mbalimbali na wanahabari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye kombano hilo la siku mbili linalofanyika mkoani Dodoma.
Pichani ni baadhi ya Wadau mbalimbali na wanahabari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye kongamano hilo la siku mbili linalofanyika mkoani Dodoma.
Wanahabari wakifuatilia mada mbalimbali zikijadiliwa ndani ya kongamano hilo .
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF,Bwa.Raphael Mwamoto,Kaimu Mkurugenzi wa Tiba na Ushauri wa NHIF,Bwa.Mkwabi Fikirini na Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) wakiwa kwenye  kongamano la tisa la Wanahabari linalofanyika kwenye moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani Dodoma .
Pichani ni baadhi ya Wadau mbalimbali na wanahabari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye kombano hilo la siku mbili linalofanyika mkoani Dodoma.
Pichani ni Mganga Mkuu wa hospitali ya Singida,Dkt.Doroth Bwajima (RMO),akizungumza mbele ya wanahabari na wadau wengine walioshiriki kongamano la tisa la Wanahabari linalofanyika kwenye moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani Dodoma kuhusiana na mada yake iliyohusu Matumizi ya Fedha za Uchangiaji (NHIF,CHF,PAPO KWA PAPO).kongamano hilo limeandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Wanahabari mbali mbali kutoka kuli ni James Paul na Asiraji Mvungi kutoka ITV.

No comments:

Post a Comment