Makamu wa Mkuu
wa Mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo ameagiza uchunguzi wa kina kufanyika
kufuatia soko la wafanyabiashara wa Vinyago na bidhaa mbalimbali za
kitalii la Maasai Market kuteketea kwa moto.
Mulongo
ambaye alifatana na kamati ya Ulinzi na Usalama alishangaa kuona maduka
hayo ambayo yapo jirani na Kikosi cha Zima Moto kushindwa kuzima moto
na kusababisha hasara kwa wananchi.
"Sitakubali
kuona uzembe unaendelea katika mkoa wetu,lazima watu wawajibishwe kwa
uzembe hasa Kikosi cha kuzima moto ambao wako mita chache na yalipo maduka haya"amesema Mulongo
Chanzo
cha moto bado hakijaweza kufahamika huku maduka hayo yapatayo 188, huku
yakiwa hayajaunganishwa na Umeme kwa lengo la kuepusha hatari ya moto
kwani bidhaa nyingi ni vinyago vinavyotengenezwa kwa mbao.
Habari picha kwa hisani ya woindeshizza blog
Watu wakiokoa baadhi ya mabaki ya Bidhaa hizo
Vijana wakionekana wakiokota baadhi ya bidhaa zilizosalia
Sehemu
ya Wafanyabiashara wa SOKO la bidhaa za utamaduni
la MT.MERU CURIOS & CRAFTS MARKET wakiwa wameduwaa bila kujua la
kufanya mara baada ya Soko hilo kuteketea kwa moto usiku
na kuunguza bidhaa zote za wafanya biashara zililopo katika soko hilo
Baadhi
ya bidhaa zilizoteketea kwa moto katika SOKO la bidhaa za utamaduni la MT.MERU CURIOS& CRAFTS MARKET ,Jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment