Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli kushoto akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Said Meck Sadiki Meli kubwa ya mizigo iliyobeba Kivuko kipya cha
MV Dar es Salaam ilipokuwa inakaribia kutia nanga katika bandari ya Dar
es Salaam.
Taaswira
ya Kivuko cha MV Dar es Salaam kama kinavyoonekana juu ya Meli kabla ya
kushushwa majini katika bandari ya Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akionesha furaha yake ndani ya Kivuko hicho cha MV Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki kulia akiwa pamoja na Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi
wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko kutoka TEMESA Eng. Japhet
Masele kuhusu vitu mbalimbali ndani ya Kivuko hicho cha MV Dar es
Salaam.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli kulia akimpongeza Mtendaji Mkuu wa Wakala
wa Huduma za Ufundi na Umeme (TEMESA) Eng. Marcellin Magesa kwa kazi
nzuri ya upatikanaji wa Kivuko hicho kipya na cha kisasa cha MV Dar es
Salaam.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwa ndani ya chumba cha Nahodha wa Kivuko hicho.
Mhandisi Masele akitoa maelezo kuhusu kamera maalumu kwenye Kivuko hicho.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akikagua boya la kujiokolea ndani ya siti mojawapo ndani ya Kivuko hicho kipya.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki wakwanza kushoto akiwa na
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli, Mtendaji Mkuu wa TEMESA Eng.
Marcellin Magesa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa
Iyombe wakiteta jambo kabla ya kuwasili kwa kivuko hicho kipya .
No comments:
Post a Comment