Mkurugenzi
Mtendaji wa EWP na Mkurugenzi wa Kinukamori Enterprises, Bw. Alpha
Phares Moshi (wa pili kushoto) akimkaribisha Mratibu Mkazi wa Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la maendeleo UNDP, Alvaro Rodriguez
alipowasili kwenye Taasisi isiyo ya kiserikali inayo shughulika na
uhifadhi wa mazingira eneo la Kinukamori, Marangu mkoani Kilimanjaro
wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na UNDP
huku akiwa amembatana na Mratibu wa Kitaifa miradi ya COMPACT mkoani
Kilimanjaro, Victoria Nderumaki (wa tatu kulia) pamoja na Mtaalam wa
Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu
(wa pili kushoto).
Na mwandishi wetu, Moshi
Taasisi
isiyo ya kiserikali inayo shughulika na uhifadhi wa mazingira eneo la
Kinukamori, Marangu mkoani Kilimanjaro Executive Wilderness Program
(EWP) inatafuta dola za marekani 30,000 kwa ajili ya kuendesha program
tatu zenye kutengeneza ajira, ujasirimali, utunzaji wa mazingira na
mvuto kwa watalii wanaokwenda kupanda mlima Kilimanjaro.
Kauli
hiyo wameitoa kwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa
Shirika la maendeleo UNDP, Alvaro Rodriguez wakati alipofanya ziara
mkoani Kilimanjaro kuangalia miradi inayofadhiliwa na Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Uongozi
wa EWP and Kinukamori Enterprises katika taarifa yao kwa Mratibu huyo,
iliyosomwa na Mshauri wao wa fedha Grace Shayo wamesema pamoja na nia
yao ya kuhakikisha maporomoko ya Kinukamori yanaendelea, kwanza kama
taasisi na pili kama mradi wa kuhifadhi mazingira ya Mlima Kilimanjaro
ambao ni sehemu ya urithi wa dunia, wakishirikiana na KINAPA wamefikiria
miradi kadhaa ambayo ikienda kwa pamoja itaendeleza eneo hilo.
Wamesema
fedha hizo zitatumika kutoa elimu ya ujasirimali kwa vijana 300
wanaoishi katika jamii ya Marangu ambao hutoa huduma mbalimbali kwa
wenyeji na pia wageni wakiwemo watalii. Kundi hilo linalotakiwa kupewa
mafunzo ni pamoja na wapagazi 50, waendesha pikipiki 100, wachuuzi 100
na walima mboga 50.
Mshauri
wa fedha wa EWP na Kinukamori Enterprises, Grace Shayo akisalimiana na
Mratibu miradi ya UNDP Kitaifa, Nehemia Mususuri aliyembata na Bw.
Alvaro Rodriguez. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa EWP na Mkurugenzi
wa Kinukamori Enterprises, Bw. Alpha Phares Moshi.
Pia
fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kuanzisha na kutoa huduma ya chakula
kwa wanaopanda mlima Kilimanjaro kwa lengo la kupunguza uchafu katika
mlima huo na wakati huo huo kuongeza ajira kwa vijana. Aidha fedha hizo
zitatumika kuanzisha kituo cha mazoezi kwa ajili ya wageni wanaotaka
kupanda mlima Kilimanjaro kujizoesha na hali ya eneo hilo kabla ya
kupanda mlima. Grace alisema shughuli zote hizo zimelenga vijana kuwa na
maeneo ya kudumu yenye ajira endelevu.
Pamoja
na kutoa ombi la kusaidiwa kupata fedha hizo, wameshukuru pia kwa
misaada iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP)
kwa kupitia COMPACT.Wamesema kama si misaada hiyo eneo hilo ambalo lina
historia ya kuharibiwa kwa mazingira yake lisingekuwa linavutia na kutoa
ajira kama ilivyo sasa.
Eneo
hilo limeboreka mazingira baada ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo ya EWP
kazi iliyofanywa na Bw. Alpha Phares Moshi ambaye kwa sasa ndiye
Mkurugenzi Mtendaji wa EWP na Mkurugenzi wa Kinukamori Enterprises
ambapo kwa kushirikiana na KINAPA na COMPACT vijana walipewa elimu
iliyowezesha kutengenezwa kwa mradi wa kuhifadhi mazingira ya mto Una
wenye maporomoko ya Kinukamori.
Bw. Alvaro Rodriguez akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye mradi huo.
Vijana
hao ambao ndio wanaoishi katika mteremko wa mlima Kilimanjaro walianza
shughuli hizo mwaka 1997 na kuanza kufikiria kuyatengeneza maporomoko ya
Kinukamori kama chanzo cha kivutio katika juhudi za kuhifadhi mto Una.
Walisema
kwa kuzingatia madhumuni ya kuanzishwa kwa mradi huo vijana na wanawake
walianza kurejesha hali ya mazingira kwa kuyaweka bora na kudhibiti
uharibifu wa ikolojia.
Kutokana
na juhudi hizo miti zaidi ya 5000 mingi ikiwa ya asili ilipandwa
kandoni mwa mto na sasa miti hiyo inatumika kutoa mafunzo na kurejesha
hali ya upatikanaji wa maji ya kutosha kwa ajili ya wananchi wa Marangu.
Aidha wanyama na ndege waliokuwa wametoweka kutokana na uharibifu wa mazingira uliokuwepo kwanza wameshaanza kurejea eneo hilo.
Pamoja
na mafanikio hayo EWP wanakabiliwa na changamoto kubwa hasa ukubwa wa
eneo la shughuli zao ambalo ni ndogo na sasa wanataka kusaidiwa kufika
hadi maeneo ya chemchem ya Soko iliyopo Kahe.
Mshauri
wa fedha wa EWP na Kinukamori Enterprises, Grace Shayo akisoma taarifa
ya taasisi yao kwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa
Shirika la maendeleo UNDP, Alvaro Rodriguez.
Aidha
wamesema wanakabiliwa na tatizo la fedha na hasa kushawishi vijana
kujikita zaidi katika masuala ya uhifadhi wa mazingira na utalii wa
kitamaduni. Naye Mwakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na
kuwapongeza EWP kwa kufanikisha kurejesha mazingira katika hali ya
kawaida katika eneo hilo amesema kwamba wataendelea kushirikiana nao
kuhakikisha kwamba shughuli za hapo zinahifadhi mazingira na kutoa ajira
kwa vijana.
Alisema
duniani nzima kwa sasa inakabiliwa na tatizo la ajira kwa vijana ambao
kutokana na kukosekana kwa ajira wanatopea katika ulevi na hivyo
kuhatarisha nguvu kazi hiyo muhimu.
Alisema
hata Tanzania pamoja na kuanza kufikiria kuwa na uchumi wa gesi, hatua
hiyo itachukua muda lakini kuna haja ya vijana wanaomaliza shule
wakawajibika katika miradi mbalimbali ya uhifadhi na maendeleo ya
kiuchumi.
Mshauri
wa fedha wa EWP na Kinukamori Enterprises, Grace Shayo akikabidhi
taarifa ya taasisi hiyo kwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la maendeleo UNDP, Alvaro Rodriguez aliyetembelea
mradi wao na kujionea maendeleo yao.
Mwakilishi
huyo pamoja na kutotoa ahadi katika ombi la taasisi hiyo amesema kwamba
wataangalia nini cha kufanya kwani alifika eneo hilo kujifunza na kuona
maendeleo kwani ana miezi miwili tu toka ameingia nchini kuwakilisha
mashirika ya Umoja wa Mataifa.Alisema amefurahishwa na maendeleo
yaliyopo na hasa kwa kuzingatia kwamba kulikuwa na tatizo la raslimali
kufanya shughuli hiyo.
Alisema
anatambua changamoto zilizopo cha ongezeko la watu, tatizo la ajira
kwa vijana na mabadiliko ya tabia nchi na kwamba wataendelea
kushirikiana na taasisi hiyo kuona kwamba changamoto hizo zinakabiliwa
na kufutwa.
Bango linaloonyesha tarehe ya kuzinduliwa kwa mradio huo wa COMPACT unaofadhiliwa na UNDP.
Baadhi ya sheria zilizowekwa kwenye maporomoko ya maji ya Kinukamori yaliyopo Marangu mkoani Kilimanjaro.
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce
Temu akiwa amefuatana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la maendeleo UNDP, Alvaro Rodriguez kutembelea
mazingira ya taasisi hiyo pamoja na vivutio vya kitalii vilivyomo kwenye
Maporomoko ya maji ya Kinukamori yaliyopo Marangu mkoani Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment