Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt.
Florens Turuka akifungua Mkutano wa Serikali na wadau wa Ukimwi kupitia utekelezaji
wa programu za ukimwi jana jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi
(TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho akizungumza na wadau mbalimbali walioshiriki Mkutano
wa Serikali na wadau wa Ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi jana jijini
Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa wadau wa Maendeleo kwenye sekta ya ukimwi
Dkt. Michelle Roland akiwasilisha mada wakati wa Mkutano wa Serikali na wadau wa
Ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi jana jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali walioshiriki Mkutano wa Serikali na wadau
wa Ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi wakifuatilia kwa makini mada
zilizokua zikitolewa kuhusu kupunguza maambukizi ya ukimwi hadi kufikia sifuri.
Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa
ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho katikati akijadili jambo na mgeni
rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka kushoto. Kulia ni Mwenyekiti
wa wadau wa Maendeleo kwenye sekta ya ukimwi Dkt. Michelle Roland.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt.
Florens Turuka aliyekaa katikati kwenye picha ya pamoja na Wadau mbalimbali walioshiriki
Mkutano wa Serikali na wadau wa Ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt.
Florens Turuka aliyekaa katikati kwenye picha ya pamoja na Wadau
mbalimbali walioshiriki
Mkutano wa Serikali na wadau wa Ukimwi kupitia utekelezaji wa programu
za ukimwi. Picha na: Genofeva Matemu - MaelezoSerikali kudhibiti ukimwi
kifikia
maambukizi sifuri
********************************************
Na: Genofeva Matemu – Maelezo
Serikali imepanga mikakati na
kusimamia juhudi zinazofanywa na kuendelezwa na wadau wa ukimwi kuhakikisha
kuwa maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi yanapungua hadi kufikia sifuri
ifikapo mwaka 2025.
Kauli hiyo imetolewa na
mwenyekiti mtendaji kutoka Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt.
Fatma H. Mrisho wakati wa mkutano wa serikali na wadau wa ukimwi kupitia
utekelezaji wa programu za ukimwi jana jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa mkutano huo
Dkt. Mrisho amesema kuwa maambukizi ya ukimwi yamepungua ukilinganisha na miaka
10 iliyopita kwani idadi imepungua kutoka waathirika laki moja na elfu
themanini hadi kufikia waathirika elfu sabini na mbili kwa sasa.
Akitoa mfano Dkt. Mrisho amesema
kuwa Mkoa wa Njombe, Shinyanga, Dar es Salaam, Mbeya na Rukwa ni mikoa ambayo
inaonyesha kuwa na idadi kubwa ya waathirika wa ukimwi hivyo kuwataka wadau wa
ukimwi kutoka mikoa hiyo kutoa elimu ya kutosha kwa jamii ili kupunguza
maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi pamoja na magojwa ya zinaa.
Akifungua mkutano huo, Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka amesema kuwa serikali imedhamiria
kuanzisha mfuko utakaokua unashughulikia masuala ya ukimwi wakati wa bajeti ya
mwaka 2015/2016 wenye lengo la kuondoa maambukizi mapya ya ukimwi nchini.
Aidha Dkt. Turuka ameitaka jamii
kutowanyanyapaa waathirika wa ukimwi bali wawapende na kuwapa moyo ili
waendelee kuwa na afya bora kwani serikali inawapigania na kuhakikisha kuwa
wanatumia dawa za kuongeza maisha ili kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa
huo.
Mkutano wa serikali na wadau wa
ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi ulianzishwa mwaka 2003
ukifuatiwa na ule wa mwaka 2006 na kuendelezwa kila baada ya miaka miwili
ambapo mkutano wa mwaka huu ni wa sita na umebeba kauli mbiu inayosema “Kwa
yale mafanikio ambayo tumeyapata mpaka sasa tunayaendeleza”.
No comments:
Post a Comment