Avunja Rekodi : Rainer Zietlof Avunja Rekodi Nyingine ya Dunia akiwa Tanzania, Kuchangia Vijiji Viwili - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 4 November 2014

Avunja Rekodi : Rainer Zietlof Avunja Rekodi Nyingine ya Dunia akiwa Tanzania, Kuchangia Vijiji Viwili


 Dereva Toka  Nchini Ujerumani Rainer Zietlof(katikati)Akizungumza na Wanahabari kuhusiana na rekodi yake ya kusafiri umbali mrefu Duniani Mara baada ya kuwasili nchini Tanzania kwenye Ofisi za Alliance Autos,Kulia ni Meneja mkuu wa Alliance Motors Bwana Wayne Mcintosh na kushoto kwake ni Meneja Masoko wa Alliance Autos Tharaia Ahmed.
******************************************
 Na Mwandishi Wetu
DEREVA raia wa Ujerumani Rainer Zietlof yuko mbioni kuvunja rekodi ya dunia ya kuendesha gari kwa kilometa 17,000 kutoka Ulaya hadi Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Zietlof alisema kuwa hiyo itakuwa ni rekodi yake ya tatu baada ya zile za awali alizovunja mwaka 2011 na 2012.
Awali alivunja rekodi baada ya safari iliyojulikana kama `Panamerica’ambayo ilimchukua kutoka Tierra del Fuego hadi Alaska kwa siku 11 na saa 17 wakati ile ya `Russtralia’ ilimtoa Melbourne, Australia hadi St.Petersburg nchini Urusi ambako alitumia saa 18.
Zietlof anayetumia gari aina ya VW Touareg V6 TDI alianza rasmi safari yake Septemba 21 mwaka huu huko North Cape nchini Norway na anatarajia kuikamilisha nchini Afrika Kusini, ambako atakuwa ametembea kwa kilometa 17,000.
Kwa mujibu wa dereva huyo, safari hiyo ndefu imempitisha katika nchi za Norway, Finland, Sweden, Denmark, Ujerumani, Jamhuri ya Czech, Slovakia, Hungary, Serbia, Bulgaria, Uturuki, Misri, Sudan, Ethiopia, Kenya na sasa Tanzania.
Dereva huyo alizungumza na wandishi wa habari katika makao makuu ya Alliance Autos iliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, na kusema kuwa atachangia  kiasi cha senti 20 za euro kwa kila kilomita, kwa vijiji nchini Tanzania na Zambia.
Mbali na kuahidi kuvichangia vijiji hivyo, Zietlot pia amesisitiza kuvitembelea vijiji hivyo atakavyo vichangia.
Aidha, amelisifia gari hilo  kutokana na uwezo wake wa kukabiliana na mazingira tofauti tofauti ya hali ya hewa kama baridi kali na joto pamoja na barabara mbovu.
Mradi huu wa kuzunguka sehemu mbalimbali za dunia kwa gari hilo umedhaminiwa na makampuni makubwa ya  magari ya Tehama na Volkswagen nchini Ujerumani, Slovakia na Afrika Kusini.
Katika safari hiyo Zietlow yuko na wasaidizi wake wawili, Marius Biela ambaye ni mpiga picha na mchukua video huku Matthias Prillwitz ni mzoefu wa mbio
za magari nchini Ujerumani.
Dereva huyo alianza safari zake za barabarani mwaka 2005 na ameoa na ana mtoto mmoja.

  Dereva Toka  Nchini Ujerumani Rainer Zietlof(Wa Kwanza Kulia)akiwaelezea jambo wanahabari hawapo pichani Kushoto kwake ni Meneja Masoko wa Alliance Autos Tharaia Ahmed
 Dereva Toka  Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akioyesha cheti cha rekodi ya dunia mbele ya wanahabari
 Dereva Toka  Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI
 Dereva Toka  Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya injini ya gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI aliyosafiri nayo kwenye nchi zaidi ya 19 Duniani

 Dereva Toka  Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya bodi ya gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI aliyosafiri nayo kwenye nchi zaidi ya 19 Duniani
 Dereva Toka  Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya sehemu ya kuweka vifaa vya akiba kwenye gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI. Kwa Picha Zaidi Bofya Hapa >>>>

No comments:

Post a Comment