Waziri
wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia,
Philippe Dongier wakikata utepe kuzindua rasmi Mpango wa Awamu ya Pili
ya Utekelezaji wa Maendeleo ya Sekta ya Maji.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Mbogo Futakamba, akisoma hotuba
katika uzinduzi rasmi wa Mpango wa Awamu ya Pili ya Utekelezaji wa
Maendeleo ya Sekta ya Maji, akiwa na Waziri wa Maji, Prof. Jumanne
Maghembe na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Philippe Dongier.
Waziri
wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, akisoma hotuba katika uzinduzi wa
Mpango wa Awamu ya Pili ya Utekelezaji wa Maendeleo ya Sekta ya Maji.
Baadhi ya Washirika wa Maendeleo wa Tanzania waliohudhuria hafla hiyo.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Maji.
Waziri
wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe,jana amezindua Mpango wa Awamu ya Pili
wa Utekelezaji wa Maendeleo ya Sekta ya Maji, kwa kipindi kingine cha
miaka 5 kuanzia Julai Mosi, 2014 mpaka Juni 30, 2019 katika Makao Makuu
ya Wizara ya Maji, Ubungo baada ya kukamilika kwa Mpango wa Awamu ya
Kwanza wa Utekelezaji wa Maendeleo ya Sekta ya Maji.
Uzinduzi
huo ulihudhuriwa na Washirika wa Maendeleo, Watumishi kutoka Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii, Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (TAMISEMI), Watumishi wa Wizara ya Maji na Taasisi zake.
“Tunapozindua
Awamu ya Pili ya Programu hii, tunajivunia mafanikio ya Awamu ya Kwanza
katika kuboresha usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji kwa
kuanzisha Bodi ya Taifa ya Maji na Bodi za Maji za Mabonde yote 9 nchini
zenye wajumbe kutoka sekta mbalimbali.
Na
pia, kuzijengea uwezo bodi hizo kwa kuzipatia watumishi pamoja na
vitendea kazi katika kuhakikisha zinatekeleza majukumu yake ipasavyo”,
alisema Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe.
Aidha,
Prof. Maghembe alisema kwamba ili kukabiliana na uharibifu wa vyanzo
vya maji unaosababishwa na shughuli za kibinadamu, tumeandaa Programu
Maalum ya Miaka 5 ya utunzaji na uhifadhi wa vyanzo vya maji kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali utakaoanza 2014/15.
Pia,
Prof. Maghembe alisema kwamba katika kutekeleza Awamu ya Pili ya
Maendeleo ya Sekta ya Maji chini ya utaratibu wa Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii Wizara imedhamiria kujenga miundombinu ya huduma bora za
maji, usafi wa mazingira na vyoo kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya
watu wengi na kuendelea kutoa mafunzo na ushauri kwenye taasisi za umma
na kaya zote za mijini na vijijini zijenge vyoo bora na kuzingatia usafi
binafsi na mazingira.
Prof.
Maghembe aliagiza kwamba zipewe kipaumbele kazi za usimamizi wa miradi
inayotekelezwa, ikamilike ndani ya muda uliopangwa kwa mujibu wa
mikataba na kuhakikisha kuwa miradi hiyo inalingana na thamani ya fedha
iliyotumika.
Naye
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Philippe Dongier aliipongeza Wizara
ya Maji kwa kutekeleza Awamu ya Kwanza ya Programu hii kubwa na
kuridhishwa na maendeleo yake mazuri. Pia, alisema kwamba kwa niaba ya
Washirika wenzake wa Maendeleo wanapendelea baadhi ya vipaumbele ikiwemo
kuweka mpango maalum wa kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa ili
kukabiliana na changamoto za uharibifu wa rasilimali za maji kwa ajili
ya kupata maji ya kutosha.
Mpango
wa Awamu ya Kwanza umefanikiwa kuongeza vituo vya kuchotea maji
vijijini, kutoka vituo 44,738 vilivyokuwa vikifanya kazi mwaka 2007 hadi
vituo 77,584 mwezi Juni, 2014 ambalo ni ongezeko la asilimia 78
ukilinganisha na lengo la awamu hii, ambalo lilikuwa ni kujenga vituo
41,900.
Vile
vile, ongezeko la wateja wapya 236,541 waishio mjini, wenye makazi yenye
jumla ya watu 2,700,000 sawa na asilimia 90 kwa kulinganisha na wateja
287,200 waliokuwa wamelengwa, wenye makazi yenye watu 3,000,000.
Mpango
wa Utekelezaji wa Maendeleo ya Sekta ya Maji, ni mpango wa miaka 20
unaotekelezwa kwa awamu na ulizinduliwa rasmi na Rais wa Tanzania, Mh.
Jakaya Kikwete, Julai Mosi, 2007 na unategemewa kukamilika ifikapo Juni,
2025.
Madhumuni
makuu ya Programu hii ni kuhakikisha kuwa Sekta ya Maji inayafikia
malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ifikapo mwaka 2025, yenye dhima ya
kuwapatia wakazi wote wa mijini huduma za maji safi na salama na
kuwapatia huduma hizo wakazi wa vijijini kwa asilimia 90.
Awamu
ya Pili ya Programu hii inakadiriwa kugharimu Dola za Marekani Trilioni
3.34, ambazo zitatokana na Bajeti ya Serikali kwa kuchangiwa na
Washirika wa Maendeleo.
No comments:
Post a Comment