Mratibu
wa mradi wa PREPARE ambaye pia ni Mwanasaikolojia wa Chuo Kikuu cha
Afya na Sayansi shirikishi cha Muhimbili, Kitengo cha magonjwa na afya
ya akili, Lusajo Kajula (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari
baada ya kukamilisha SAMPULI tathmini ya matokeo ya mradi wa PREPARE
uliokuwa na lengo la kuangalia uwezekano wa vijana kupunguza ngono
mwishoni mwa wiki kwenye kituo cha maelezo ya afya Muhimbili katika
idara ya magonjwa ya akili. Kulia ni Mtathmini kiongozi wa mradi huo,
Mrema Kilonzo.
Na Mwandishi wetu
SAMPULI
tathmini ya matokeo ya mradi wa PREPARE uliokuwa na lengo la kuangalia
uwezekano wa vijana kupunguza ngono, imebainisha haja ya elimu ya afya
ya uzazi kukabili hali ya sasa ya tabia hatarishi zinazowakabili vijana
wadogo.
Matokeo
ya awali ya mradi yalionesha kuwa asilimia 10 ya vijana wenye umri wa
miaka 12 mpaka 14 ambao ni darasa la tano na sita waliofanyiwa utafiti
walikuwa wameshawahi kufanya ngono na asilimia kubwa ikiwa ni kwa
kutumia njia ya haja kubwa.
Kauli
hiyo imetolewa na mmoja wa watafiti wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
shirikishi cha Muhimbili,Kitengo cha magonjwa na afya ya akili, Lusajo
Kajula.
“Vijana
wengi walionekana wakifanya ngono ya uke na ya mdomo ikifuatiwa na
ngono ya njia ya haja kubwa Kwa wale ambao wameshawahi kufanya ngono,
asilimia 6.3 wamefanya ngono ya njia ya haja kubwa wakati asilimia 93.7
hawajawahi.”
Aidha alisema utumiaji wa kondomu ulionekana kuwa mdogo kwa vijana wadogo ambao wameanza kufanya ngono.
“Asilimia 68 ya wale walioanza kufanya ngono hawajawai kutumia kondomu kabisa wakati asilimia 32 wamewahi kutumia kondomu.”
Alisema
utafiti huo ni sehemu ya utafiti wa miaka minne ulioshirikisha Vyuo
Vikuu vya Makerere cha Uganda, Cape Town na Limpopo vya Afrika Kusini,
Bergen na Oslo vya Norway, Maastricht cha Uholanzi na Sussex cha nchini
Uingereza.
Mtathmini
kiongozi wa mradi huo, Mrema Kilonzo akifafanua jambo kwa waandishi wa
habari (hawapo pichani) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Alisema
utafiti umeonesha haja ya kutolewa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana
wadogo ambao bado hawajaanza ngono ili kuchelewesha kuanza ngono kwa
mfumo wa kisaikolojia ili waweze kujitambua na kuacha kufuata nadharia
za kisayansi pekee ambazo ndizo zinazotumika katika shule mbalimbali
kuwaeleza mabadiliko ya miili yao.
Katika
utekelezaji wa utafiti huo idadi ya wanafunzi 5,099 walichaguliwa
mwanzoni mwa mradi kufanyiwa utafiti huo ambapo wanafunzi 4783 (asilimia
93.9) walifuatiliwa kwa miezi 6 na wengine 4370 (asilimia 85.8)
walifuatiliwa kwa miezi 12.
Utafiti
ulionesha elimu inayojishughulisha na masuala ya ujinsia na afya ya
uzazi kwa vijana wadogo itumie mtazamo mpana utakaoleta mabadiliko ya
msingi kwenye misingi ya virekebisho vya mabadiliko ya tabia.
Mradi
huo wa PREPARE ulitekelezwa kwenye shule 38 kutoka manispaa ya
Kinondoni zilizochaguliwa kwa kutumia taratibu sampuli mtawanyiko
zilizopangwa katika makundi mawili ya shule za mwingilio yaani
ilikotolewa elimu hiyo zilizokuwa 19 na za kulinganisha zilizokuwa 19.
Ili
kuweza kupata matokeo yaliyokusudiwa mradi ulitoa mafunzo kwa walimu
watano wakufunzi wa wakufunzi; ulitoa mafunzo kwa walimu watekelezaji
76, na waelimishaji rika wanafunzi 132 na kuelekeza watoa huduma 8 wa
afya katika kliniki za huduma rafiki kwa vijana ili kutekeleza
muingiliano.
Tathmini
iliyotoa majibu ya jinsi utendaji unavyoendelea na ya matokeo
ilihusisha shule zote na wanafunzi zaidi ya 6,000 waliowekwa kwenye
muingiliano, huku uchambuzi wa tathmini ukihusisha wanafunzi wenye umri
wa miaka 12-14, wenye kujua kusoma na kuandika.
Matokeo
yaliyotathminiwa ni Mabadiliko katika masuala ya ngono (kuanza ngono)
na Kutumia kondomu wakati wa kujamiiana kwa wale waliokwisha anza ngono.
Kwa
wastani mradi uliona kwamba mwingilio wa PREPARE ulipunguza uwezekano
wa vijana wadogo (wavulana na wasichana) kuanza ngono na kuongeza
uwezekanao wa kutumia kondomu kwa wale walioanza.
Baadhi
ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo. Kushoto ni mwandishi
wa habari wa gazeti la Mwananchi, Vicky Kimaro akiuliza swali kwenye
mkutano huo.
Hata
hivyo, katika utekelezaji wa mradi mabadiliko katika uchukuaji wa hatua
yalionekana zaidi miongoni mwa wasichana waliopata mwingilio
ukilinganisha na wale ambao hawakupata mwingilio.
Uchukuaji
wa hatua ulisababisha tabia ya kutumia kondomu miongoni mwa wanafunzi
wa kiume lakini siyo miongoni mwa wanafunzi wa kike.
“Kimsingi
tunataka kuwaambia wanahabari kuwa miongoni mwa mafanikio makubwa ya
mradi wa PREPARE ni kuchelewesha kuanza ngono miongoni mwa wanafunzi wa
kiume na wa kike wenye umri wa miaka 12-14 katika mkoa wa Dar es Salaam,
Tanzania;
“Kuongeza
uchukuaji wa hatua ulio chanya katika kutumia kondomu kwa jinsia zote
na taarifa za ongezeko la utumiaji wa kondomu miongoni mwa vijana wa
kiume. “
Mradi
huu uliofadhiliwa na Umoja wa Nchi za Ulaya, Programu ya utafiti wa
afya umelenga kuangalia mwingilio ulio katika misingi ya utamaduni na
jinsia, endelevu, kijamii ili kukuza ujinsia na afya ya uzazi miongoni
mwa vijana wenye umri kati ya miaka 12-14 kwa kutumia shule kama njia ya
kufundishia.
No comments:
Post a Comment