ELIMU ZETU :TAASISI YA WAMA NA UNICEF WAANDAA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WALIMU WA SEKONDARI WAMA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 17 September 2014

ELIMU ZETU :TAASISI YA WAMA NA UNICEF WAANDAA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WALIMU WA SEKONDARI WAMA


 Mkuu wa Kitengo cha Uragibishi na Mawasiliano kutoka Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Philomena Marijani akiwakaribisha walimu na wageni waalikwa wakati wa sherehe ya ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama iliyoko katika Kijiji cha Nyamisati huko Wilayani Rufiji yaliyofanyika shuleni hapo jana.
 Baadhi ya walimu wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama wakifuatilia kwa makini  hotuba ya ufungunzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu haokatika masuala ya jinsia na stadi za maisha. Hotuba hiyo ilikuwa ikitolewa na Mkurugenzi wa Elimu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Dkt. Mikidadi Alawi (hayupo pichani)
 Mwezeshaji wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama Ndugu Anitha Masaki kutoka Shirika la FAWE (Forum For African Women Educationalists-Tanzania Chapter) akitoa moja ya mada zake mara tu baada ya ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo shuleli hapo.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama mara baada ya ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo. PICHA NA JOHN  LUKUWI.
***************************************
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Walezi wameaswa kuwaelimisha, kuwalinda, kuwaandaa na kuwajali watoto wa kike namna ya kupambana na changamoto mbalimbali za kijinsia zinazowakumba watoto hao wakati wakiwe shuleni na hata nyumbani wa likizo.
Kauli hiyo imetolewa na Mwezeshaji kutoka TUSEME wa masuala ya Ufundishaji ambao ni Rafiki Kijinsia Anita Masaki wakati wa semina ya siku tano kwa walimu na watumishi wasio waalimu wa  Shule ya Wasichana ya WAMA-Nakayama  iliyopo kijiji cha Nyamisati walayani Rufiji mkoa wa Pwani.
Anita amewataka walezi hao kutambaua dhamana waliyopewa na wazazi wa watoto hao na taifa kwa ujumla ya kuwaandaa vema wanafunzi hao kitaaluma na watambue umuhimu wao wenyewe na kwa taifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Elimu kwa mtoto wa kike wa taasisi ya WAMA Mikidadi Alawi akimkaribisha Mwezeshaji wa semina hiyo alitoa taarifa fupi ya shule hiyo kuwa ina idadi ya wanafunzi 400 tangu kuanzishwa kwake ambapo kwa sasa wapo wanafunzi 363.
Alawi alisema kuwa shule ya WAMA-Nakayama ilianzishwa kwa lengo la kuwalea watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu ambapo wanatoka mikoa yote nchini.
Naye Mlezi wa wanafunzi shuleni hapo Sarah Ngonde amesema kuwa wamenufaika na semina hiyo kwa kuwa imekuja wakati mwafaka kuimarisha maarifa yao ya namna ya kuwalea wanafunzi hao ili kuwasaidia wafikie malengo yao na hatimaye kuwa raia wema nchini.
Sarah alisema kuwa wanaamini watakapo maliza semina hiyo watakuwa wanajua zaidi namna ya kuangalia masuala ya kijinjsia katika shuleni hapo na hata watakapokuwa na familia zao nyumbani.

Shule ya Wasichana ya WAMA-Nakayama inayomilikiwa na taasisi isiyo ya serikali ya WAMA inatoa elimu ya sekondari kwa wasichana kidato cha kwanza hadi sita ilizinduliwa rasmi Septemba 24, 2011 na Rais wa Serlikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein.

No comments:

Post a Comment