Kaimu
Mkurugenzi Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Mary Meela
akiwaeleza waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu Mikakati wanayoweka ya
kuendelea kudhibiti ubora wa bidhaa nchini ikiwemo kuimarisha ukaguzi kwenye
vituo vya mipakani mwa nchi,Kulia ni Afisa Habari Wa Idara ya Habari Bw. Frank
Mvungi.
Afisa
Uhusiano wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Roida Andusamile
akitoa wito kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuendelea
kuelemisha umma kuhusu madhara ya matumizi ya nguo za mdani za mtumba.
Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Udhibiti Ubora wa Shirika hilo Bi. Mary Meela.
*********************************
Frank Mvungi-Maelezo
Shirika la viwango Tanzania (TBS) linatarajia kuajiri watumishi 200 katika harakati za kuimarisha utendaji wa shirika hilo.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa udhibiti ubora wa shirika hilo Bi Mary
Meela wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es
salaam.
Akifafanua
Meela amesema watumishi watakaoajiriwa watasaidia kuimarisha utendaji
kazi wa shirika hilo hasa katika kufanya ukaguzi na kuhakisha tatizo la
bidhaa hafifu linapungua au kuondolewa kabisa.
Aidha
Bi. Meela alisema kuwa Shirika limeweza kuweka wakaguzi kwenye vituo 5
ambavyo ni Sirari, Namanga, Taveta, Horohoro, Bandari za Tanga na Dar es
salaam na kuweka wakaguzi kwenye vituo vya bandari kavu (ICD).
Akizungumzia
kuhusu utumiaji wa nguo za ndani za Mtumba Bi. Meela amewataka
watanzania kuwa mstari wa mbele kupinga matumizi ya nguo hizo kwani zina
madhara kiafya kwa watumiaji na wataendelea kufanya ukaguzi wa nguo
hizo na kuziteketeza pindi zinapopatikana.
Shirika
la viwango lilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 3 ya mwaka 1975, kasha
kuundwa upya mwaka 2009 sheria ambayo imelipa shirika uwezo mkubwa zaidi
wa utayarishaji viwango na kusimamia utekelezaji wake.
No comments:
Post a Comment