Mbunge
wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa (kulia) akikabidhi ahadi ya bati
100 alizokuwa ameziahidi mbunge aliyepita marehemu Dr Wiliam Mgimwa kwa
viongozi wa kijiji cha Mangalali kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya
madarasa shule ya msingi Lukwambe hadi sasa ni asilimia 90 ya ahadi
binafsi za mbunge aliyefariki zimetekelezwa jimbo la Kalenga na mbunge
Mgimwa.
|
mbunge wa Kalenga Godfrey Mgimwa akiongoza viongozi kutembelea ujenzi wa zahanati kijiji cha Mangalali |
Diwani wa kata ya Ulanda kulia akitoa ufafanuzi kwa mbunge wa jimbo la Kalenga Bw Mgimwa kuhusu maendeleo ya ujenzi wa zahanati kijiji cha Mangalali |
Katibu wa mbunge Mgimwa kulia Bw Martine Simangwa kulia akiteta jambo na mbunge Mgimwa. |
Mwananchi wa kijiji cha Mangalali akisalimia na mbunge wa jimbo la Kalenga Bw Godfrey Mgimwa |
Mbunge Mgimwa akidua sanjari na wananchi wa kijiji cha Mangalali |
Mmoja kati ya wananchi wa kijiji cha Mangalali akimpongeza mbunge Godfrey Mgimwa kwa utendaji kazi mzuri |
Katibu wa Mgimwa akiwaonya wana CCM wanaojipitisha jimboni kwa sasa |
Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Mangalali wakiwa katika mkutano wa mbunge wao Bw Mgimwa |
.......................................................................................................
Na Matukiodaima.co.tz
MBUNGE
wa jimbo wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa ajipongeza kutumia
kiasi cha zaidi ya Tsh milioni 68 kwa ajili ya kufanikisha
utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na mbunge aliyefariki Dr Wiliam
Mgimwa kwa asilimia 90 kwa muda wa miezi mitatu pekee .
Akizungumza
na wananchi wa kijiji cha Mangalali baada ya kukamilisha ahadi
ya bati 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya
msingi Lukwambe , mbunge Mgimwa alisema kuwa alianza kutekeleza
ahadi hizo hata kabla ya kuapishwa bungeni na hadi sasa bado
asilimia 10 pekee ya utekelezaji wa ahadi zilizoachwa na mbunge
aliyefariki dunia mwanzoni mwa mwaka huu marehemu Dr Mgimwa ambae
alikuwa ni babake mzazi.
"
Ni jambo la kumshukuru mwenyezi Mungu kwani ahadi zilizokuwa
zimetolewa na mbunge aliyefariki dunia marehemu Dr wiliam Mgimwa
zilikuwa ni asilimia 100 na hadi mnanichangua kuwa mbunge ahadi hizo
zilikuwa bado kutekelezwa na ndio sababu ya mimi katika kampeni
kutoahidi ahadi mpya zaidi ya kuzipokea zile zilizoachwa na baba
ambazo kimsingi nilizipokea .......ila kwa sasa ahadi hizo
nimetekeleza kwa asilimia 90 bado asilimia 10 pekee ambazo hadi mwakani
nitakuwa nimezimaliza kikubwa naomba mzidi kuniombea uzima" alisema
mbunge Mgimwa.
Alisema
kuwa hakuweza kuahidi ahadi mpya wakati wa kampeni hizo za uchaguzi
mdogo jimboni humo kutokana na kuwepo kwa ahadi nyingi ambazo
zilikuwa zimetolewa na mbunge aliyepita na zilikuwa bado kutekelezwa
na muda wa utekelezaji ulikuwa bado hivyo aliamua kuzichukua zote
kama zilivyo na kuanza kuzifanyia kazi moja baada ya nyingine .
Mbunge
Mgimwa alisema kuwa ahadi hizo zinazotekelezwa ni zile ahadi
binafsi ambazo mbunge aliyepita alikuwa amezitoa ila zipo ahadi mbali
mbali ambazo zimo katika ilani ya CCM ambazo pia zimeendelea
kutekelezwa kwa nguvu kubwa .
Hata
hivyo alisema kuwa ahadi ambazo zimetekelezwa kwa asilimia 90 ambazo
zilikuwa ni ahadi binafsi ni pamoja na elimu ,afya na uchangiaji wa
vikundi vya Vicoba pamoja na uanzishwaji wa vikundi hivyo pia katika
sekta ya michezo na huduma nyingine za kijamii kama upelekaji wa
umeme katika maeneo ya kata ya Mgama na Magulilwa zoezi hilo
linaendelea ambayo ahadi hiyo ya umeme ipo katika ilani ya CCM
pamoja na zile za huduma za maji vijijini ambazo baadhi ya maeneo mradi
kata ya Maboga na kata ya Lumuli wa maji unatekelezwa .
Pia
alisema kuwa bado anautamani ubunge wa jimbo hilo la Kalenga kwa
mwaka 2015 -2020 hivyo kamwe hatawaangusha wana Kalenga kwa kipindi
hiki cha miaka miwili alichopewa hadi 2010.
"
Ndugu zangu hii nafasi ya ubunge mimi nimeipata mwishoni ila
sikutaka kuwaangusha nilitaka kuwaonyesha utendaji wangu na kamwe
sitakuwa mbali na ninyi wananchi wangu nitakuwa bega kwa bega
kuhakikisha jimbo la Kalenga linapata maendeleo na linakuwa ni jimbo
la mfano katika maendeleo kule bungeni kutokana na umri wangu
wabunge wananiita bwana mdogo ila kiutendaji kweli ni bwana mkubwa
kwani kati ya wabunge zaidi ya 300 bungeni mimi ni mmoja kati ya
wabunge tuliochanguliwa kuingia katika kamati ya bunge ya bajeti ya
serikali " alisema mbunge Mgimwa .
Awali
katibu wa mbunge huyo Martine Simangwa aliwaonya wana CCM ambao
wameendelea kujipitisha katika jimbo hilo na kuwa kwa kufanya hivyo
ni kutowatendea haki wananchi wa jimbo la Kalenga ambao kwa sasa
wameshikamana na wapo tayari kuona maendeleo na sio kampeni za
uchaguzi wa mwaka 2010.
"
wapo baadhi ya wana CCM bila haya wameendelea kujipitisha kwa
wananchi na kuponda utendaji huu mzuri wa mbunge Godfrey Mgimwa
....sasa wananchi nawaombeni sana msidanganyike na watu hao kwa sasa
mbunge ni Godfrey Mgimwa wakija na kuwapa pesa chukueni ila msikubali
kugawanywa kwa misingi ya pesa kubalini kuungana katika misingi ya
kimaendeleo"
Kwa
upande wao wananchi hao walieleza kufurahishwa na utendaji mzuri wa
mbunge wao Mgimwa na kuwa kamwe hawatakubali kudanganyika na kuwa
wamejipanga kumchukulia fomu mwakani ili kuwaongoza vipindi vingine
viwili zaidi baada ya kuona utendaji wake mzuri.
No comments:
Post a Comment