Mkurugenzi
wa MBEPAU, Jane Lawa, akizungumza wakati wa kutambulisha mradi wa
kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake,kwa Halmashauri ya
Wilaya ya Mbeya.
Mjumbe
wa bodi ya MBEPAU, Philimon Mwansasu, akimkaribisha mgeni rasmi, wakati
wa kutambulisha mradi wa kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa
wanawake,kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Mgeni
rasmi,Afisa Tarafa ya Usongwe, Felix Lyaniva, akizungumza wakati wa
kutambulisha mradi wa kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa
wanawake,kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Baadhi ya washiriki wa semina ya kutambulisha mradi wakifuatilia kwa makini.
Picha ya pamoja baada ya semina.
KITUO
cha Msaada wa kisheria kwa wanawake(MBEPAU) kimezindua mradi mpya
kuhusu kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Wanawake katika
Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Utambulisho
wa mradi huo ulifanyika jana katika ukumbi wa Royal Tughimbe uliopo
Mbalizi na kuwashirikisha wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia ambao ni
viongozi wa dini, watendaji wa Kata, viongozi na mila na watu mashuhuri.
Awali
akimkaribisha mgeni rasmi katika utambulisho huo, Mkurugenzi wa MBEPAU,
Jane Lawa, alisema lengo la kuanzishwa kwa kituo hicho ilikuwa ni
kuwasadia wanawake na watoto katika sheria zinazowabagua na
kuwakandamiza.
Alisema
pia kupitia MBEPAU wanawake na watoto wanaweza kuzitambua sheria na
kuzilinda na kuzitetea haki zao baada ya kuzifahamu na kuzitambua.
Aliongeza
kuwa hayo yote yametokana na gharama kubwa ya Wanasheria katika
kushughulikia malalamiko yanayopelekwa wanawake wengi wasiojiweza na
utaratibu wa kutoza fedha kabla ya huduma ufanywao na wanasheria.
Mama
Lawa alisema katika Mradi huo mpya chini ya ufadhili wa Legal Services
Facility(LSF) ya nchini Denmark utafanyika kwa miezi 30 kwa gharama ya
shilingi Milioni 200.
Alisema malengo ya Mradi ni kuongeza ufikiaji wa huduma za kisheria kwa wanawake na wanaume wilayani Mbeya, kuwajasirisha wanawake
kuweza kutumia mifumo ya kulinda haki zao na kuongeza mwitikio wa jamii
katika kushughulikia matukio ya ukatili wa kijinsia wilayani Mbeya.
Alisema
kutokana na mradi huo wasaidizi wa kisheria 50 wamepata mafunzo juu ya
ulinzi wa haki za wanawake na utoaji wa huduma za kisheria kwa
Halmashauri za wilaya Mbeya na Jiji.
Aliongeza
kuwa viongozi 50 wa jadi, kisiasa na dini pia wamepata mafunzo juu ya
ukatili wa kijinsia pamoja na utambulisho wa mradi kwa wadau 80 kutoka
Halmashauri ya wilaya Mbeya na Jiji.
Awali
akizindua mradi huo, Mgeni rasmi wa tukio hilo, Katibu Tarafa wa tarafa
ya Usongwe, Felix Lyaniva, alilipongeza Shirika la MBEPAU kwa juhudi
zao za kupinga ukatili wa kijinsia na kutoa kipaumbele kwa Halmashauri
ya Wilaya ya Mbeya.
Alisema
ili juhudi hizo ziendelee kuungwa mkono ni vema washiriki wa Semina
hiyo wakafikisha elimu kwa wananchi katika ngazi za chini ili wawe na
uelewa juu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na msaada wa
kisheria.
Aidha
alitoa wito kwa Wamiliki wa Asasi za kiraia kufikisha huduma zao
vijijini kwa kuwa wanaowalenga zaidi ni wanawake na watoto waishio
vijijini hivyo ni bora kujenga ofisi huko huko kuliko kujikita mijini
tu.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment