Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya Uchina, Bw. Jiang Zhigang (Katikati) akisisitiza jambo
wakati walipokuwa na mazungumzo na Uongozi wa Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango. Kushoto ni Mtafiti Kutoka ‘State Information Center’, Bw. Chen
Qiang na Kulia ni Bw. Zhao Bingjie, Mhandisi Mwandamizi kutoka ‘Railway
Third Survey and Design Institute Group’.
Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya Uchina, Bw. Jiang Zhigang (Katikati) akiongoza mjadala
wakati wa majadiliano na na Uongozi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
(Hawapo pichani) juu ya uwezekano wa Benki hiyo kufadhili baadhi miradi
ya maendeleo nchini.
Naibu
Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (anayeshughulikia
Biashara za Kimataifa na Mashirikiano ya Kiuchumi), Bw. Paul Sangawe (Kulia) akibadilisha mawazo na Ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Uchina (Hawapo pichani) wakati walipotembelea Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango .
Wakili
wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Wakili Nyanzala Nkinga (Katikati)
akifafanua jambo kwa mmoja kati ya wajumbe wa majadiliano, Bibi Martha Luanda (Kulia). Kushoto ni Bi. Gloria Ngowi.
Picha na Saidi Mkabakuli
******************************************
*Yazungumzia uwezekano wa kugharamia utekelezaji wa miradi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025
Na Saidi Mkabakuli
Ugeni
kutoka Benki ya Maendeleo ya Uchina umetembelea Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango kwa minajili ya kuja kujadiliana juu ya uwezekano wa kugharamia
miradi ya maendeleo kwa upande wa barabara, kilimo na nishati ili
kuiwezesha Tanzania kufikia lengo lake la kuwa nchi ya uchumi wa kati
kufikia mwaka 2025.
Ugeni
huo unaongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Bw. Jiang Zhigang
utatembelea wizara mama zinazosimamia miradi itakayogharamiwa na Benki
hiyo ambazo ni pamoja na Wizara ya Kilimo, Wizara ya Uchukuzi na Wizara
Nishati na Madini.
“Tumekuja
Tanzania kwa ajili ya kukagua na kujionea maendeleo ya sekta za
kipaumbele ambazo tutagharamia ili kupata uelewa wa gharama halisi ya
miradi hiyo,” alisema Bw. Zhigang.
Kwa
mujibu wa makubaliano ya awali yaliyofanyika mwezi Julai, 2012 kati ya
taasisi hizi mbili, Tume ya Mipango imekubali kupatiwa utaalamu elekezi
kwenye maeneo hayo wenye lengo la kukuza ushirikiano wa kihistoria baina
ya nchi hizo.
Wakati
huo huo, imebainika kuwa Tanzania imekuwa kinara katika kuvutia
uwekezaji wa ndani na nje ya nchi miongoni mwa nchi zilizo chini ya
Jangwa la Sahara kutoka asilimia 18 ya Pato la Taifa (GDP) kwa mwaka
2002 hadi kufikia asilimia 34 kwa mwaka 2013.
Hayo
yamewekwa wazi na Naibu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango (anayeshughulikia Biashara za Kimataifa na Mashirikiano ya
Kiuchumi), Bw. Paul Sangawe wakati akiwasilisha mada ya Hali ya Uchumi
wa Tanzania wakati Ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Uchina
ulipoitembelea Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
“Tunajitahidi kuvutia uwekezaji wa ndani na nje ya nchi, kwa mfano, mwaka 2003 tuliweza kuvutia uwekezaji kutoka nje ‘Foreign Direct Investment (FDI)’ wa jumla ya Shilingi za Kimarekani milioni 308.2, na mwa 2013 zilifikia Shilingi za Kimarekani milioni 1,872.4,” aliongeza.
No comments:
Post a Comment